Kocha wa  Azam, Aristica Cioaba ameonekana kuijenga  safu yake ya ulinzi kwenye mazoezi ya kikosi hicho kuelekea mchezo wa Jumamosi watakaocheza dhidi ya Yanga.
Katika mazoezi hayo ambayo Azam imeyafanya kwenye uwanja wake wa Azam Complex, Chamazi walionekana kuchezea zaidi mpira kwa  masharti ya kuugusa mara mbili hadi tatu.
Mara kadhaa Mromania huyo alikuwa akitoa maelekezo kwa walinzi wake, Daniel Amoah, Yakubu Mohammed, Aggrey Morris na Bruce Kangwa ambao walicheza pamoja.
Pia, Azam imefanyia kazi namna ya kupanga mashambulizi yake kuanzia kwenye eneo lake hilo la nyuma huku viungo wakiwatengenezea nafasi washambuliaji wa kikosi hicho.

Share To:

msumbanews

Post A Comment: