Tetemeko la ardhi ya ukubwa wa 6.2 katika vipimo vya Richter limetikisa maeneo ya katikati mwa Italia na kufukua watu chini ya vifusi, maafisa wa Italia wamesema

Tetemeko hilo lilitokea mwendo wa saa tisa na dakika thelathini na sita usiku saa za Italia (01:36 GMT), 76 km (maili 47) kusini mashariki mwa mji wa Perugia, katika kina cha 10km (maili sita) chini ya ardhi, taasisi ya USGS imesema.
Meya wa mji mmoja ulio eneo hilo ameambia kituo kimoja cha redio kwamba “nusu ya mji imetoweka”. Mjini Roma, baadhi ya majumba yalitikisika kwa sekunde 20, ka mujibu wa gazeti la La Repubblica.
Mji wa Venice pia uliathiriwa.
Kitovu cha tetemeko hilo kilikuwa katika mji wa Norcia, karibu na Perugia. Waziri mkuu wa Italia, Matteo Renzi, amesema serikali yake inaendelea kuwasiliana na taasisi za kiraia la ulinzi wa nchi hiyo.
Meya wa mji wa Amatrice Sergio Perozzi ameambia kituo cha redio cha serikali cha RAI kwamba mji huo umeharibiwa vibaya.
“Barabara za kuingia na kutoka mjini hazipitiki. Nusu ya mji imeharibiwa. Watu wamefukiwa chini ya vifusi… kumetokea maporomoko ya ardhi na kuna daraja moja ambalo huenda likaporomoka,” amesema.
Shirika la kulinda raia Italia limeeleza tetemeko hilo kuwa “mbaya”. Tetemeko hilo awali lilikisiwa kuwa la ukubwa wa 6.4. Lilifuatwa na mitetemeko mingine mikubwa, gazeti la
La Repubblica limeripoti.
USGS wamesema uharibifu huenda ukawa mkubwa. Mwaka 2009, tetemeko la ardhi la nguvu ya 6.3 lilitokea eneo la Aquila, na kusikika pia katika mji wa Roma. Watu zaidi ya 300 walifariki.
Share To:

msumbanews

Post A Comment: