Ndege mbili za kivita za Marekani zenye uwezo wa kubeba silaha za nyuklia, B-1 Lancer, zimepaa juu ya anga ya Korea Kusini, siku chache baada ya Korea Kaskazini kufanya jaribio la tano la silaha za nyuklia.

Ndege hizo zilipaa si mbali sana kutoka ardhini juu ya kituo cha kijeshi kinachopatikana kilomita 77 kutoka mpaka wa Korea Kaskazini na Korea Kusini.
Marekani imeitahadharisha Korea Kaskazini kwamba hatua kali zitachukuliwa dhidi ya taifa hilo baada ya kufanyika kwa majaribio hayo ya bomu Ijumaa.

Jaribio hilo la Pyongyang ndilo kubwa zaidi kuwahi kutekelezwa na taifa hilo.
'Ndege aina ya B-1 zina uwezo wa kubeba makombora yenye mabomu ya nyuklia au mabomu ya nyuklia yenyewe yenye uwezo wa kuharibu hata mahandaki.

Operesheni hiyo ya kupaa kwa ndege ilikuwa imepangiwa kufanyika Jumatatu lakini ikacheleweshwa kutokana na hali mbaya ya hewa Guam, eneo ambalo ndege hizo hukaa. 
Share To:

msumbanews

Post A Comment: