MAGARI YA MWENDO KASI DODOMA.

 

Baada ya kuanza kwa mafanikio kutoa huduma za usafiri katikati ya Jiji la Dar es Salaam, mabasi ya mwendokasi sasa yanatakiwa yatue mjini Dodoma.

Mbunge wa Kilolo mkoani Iringa, Venance Mwamoto ameishauri Serikali kuweka mpango wa kujenga njia za mabasi hayo ili kuepuka msongamano unaoweza kutokea baada ya Serikali kuhamia.

 

Mwamoto amesema tangu Serikali itangaze kuhamia Dodoma kumekuwa na ongezeko la watu wanaohitaji maandalizi ya huduma mbalimbali.

“Serikali isisubiri Dodoma iwe kama Dar es Salaam ili tuanze kuhangaika, mabasi ya mwendokasi yatasaidia ujenzi wa uchumi kwa kasi kwa sababu watu hawatatumia muda mrefu barabarani kama ilivyo kwa Dar es Salaam, hasa maeneo yasiyo na usafiri huo,” amesisitiza.

Akizungumza na wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali za Mitaa na Tawala za Mikoa (LAAC) walipotembelea mradi huo hivi karibuni, Mkurugenzi Mtendaji wa Dart, Ronald Rwakatare alisema hivi sasa wapo kwenye mkakati wa kuendelea na ujenzi wa barabara za  mwendokasi awamu ya pili jijini Dar es Salaam.

Share To:

msumbanews

Post A Comment: