Thursday, 11 July 2019

TANZANIA YAKABILIWA NA UPUNGUFU WA SAMAKI TANI 350,000

 Naibu waziri wa Mifugo na Uvuvi Abdallah Ulega Ulega pamoja na  Naibu Waziri wa Kilimo maliasili na Usalama wa Chakula Bi Marjolyn Sonnema kutoka nchini Uholanzi wakitia saini makubaliano ya mashirikiano baina ya serikali ya Tanzania na nchi ya Uholanzi katika Nyanja za maendeleo ya ufugaji wa Samaki na Kuku
   Naibu waziri wa Mifugo na Uvuvi Abdallah Ulega Ulega pamoja na  Naibu Waziri wa Kilimo maliasili na Usalama wa Chakula Bi Marjolyn Sonnema kutoka nchini Uholanzi wakibadilishana nyaraka mara baada ya kutia saini.
  Naibu waziri wa Mifugo na Uvuvi Abdallah Ulega Ulegaakiongea na waandishi wa habari mara baada ya kutia saini nyaraka hizo za makuliano mashirikiano baina ya serikali ya Tanzania na nchi ya Uholanzi katika Nyanja za maendeleo ya ufugaji wa Samaki na Kuku

Naibu Waziri wa Kilimo maliasili na Usalama wa Chakula Bi Marjolyn Sonnema kutoka nchini Uholanzi akimkabidhi Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo na Mifugo, Elisante Ole Gabriel   zawadi  ambayo wametoka nayo nchini uholanzi.


Na Woinde Shizza Michuzi Tv,Arusha


Tanzania ina  Upungufu wa Tani zipatazo 350,000  za Samaki kwa mwaka huku mahitaji yakiwa ni Tani 700,000 ambapo kwa mwaka kiasi cha tani  350,000  kinazalishwa,hivyo watanzania wametakiwa kuchangamkia fursa ya uzalishaji ili kufikia malengo ya mahitaji ya samaki.
Kauli hiyo imeelezwa jijini Arusha na Naibu waziri wa Mifugo na Uvuvi Abdallah Ulega wakati wa kutiliana saini makubaliano ya mashirikiano baina ya serikali ya Tanzania na nchi ya Uholanzi katika Nyanja za maendeleo ya ufugaji wa Samaki na Kuku.
Ulega amesema kuwa ushirikiano huo wa kimaendeleo na nchi ya Uholanzi umefikia miaka zaidi ya 40 katika njanja mbali mbali,ikiwemo kilimo cha Mboga mboga,Viazi Mviringo, Ufugaji wa kuku na Samaki yanayosaidia kuongeza uzalishaji wa protini na mapato kwa Taifa kwa ujumla.
Amesema kuwa Tanzania inauhitaji mkubwa wa protini inayotokana na samaki na kuku ndio maana wamekubaliana na Taifa hilo la uholanzi kuweza kuboresha Nyanja hizo kwa lengo la kutoa elimu kwa wafugaji na wakulima wa mazao ya samaki.
“Kama nchi tumejipanga kuhakikisha ukuaji wa sekta ya ufugaji wa Samaki na kuku unakuwa kwa kiasi kikubwa kuongeza Pato la taifa kutoka asilimia 9 tunazochangia katika pato la taifa”
Amesema serikali itaendelea kushirikiana na sekta binafsi katika kuhakikisha kwamba Uzalishaji wa kuku na Ufugaji wa samaki unaboreshwa na kuona viwanda vya kuchakata mazao hayo kuondoa changamoto mbali mbali ili kufikia malengo ya uzalishaji na kuondoa upungufu wa uhitaji wa soko.


Kwa Upande wake Naibu Waziri wa Kilimo maliasili na Usalama wa Chakula Bi Marjolyn Sonnema amesema kuwa Ushirikiano huo utasaidia kuboresha sekta ya ufugaji wa Samaki na kuku na kuinua vipato vya wafugaji wa samaki na kuku hususani katika sekta binafsi na jamii kwa ujumla.
Amesema kuwa vile vile uboreshaji huo wa uzalishaji wa kuku na samaki utafanywa zaidi na sekta binafsi kwa kuwapa uwezo ili kuongeza uzalishaji na mapato kuongeza mnyororo wa thamani wa uazalishaji wa mazao hayo kwa wafugaji wa ukanda wa kaskazini.

No comments:

Post a Comment