Naibu waziri wa Mifugo na Uvuvi
Abdallah Ulega
Ulega pamoja na
Naibu Waziri wa Kilimo maliasili na Usalama wa Chakula Bi
Marjolyn Sonnema
kutoka nchini Uholanzi wakitia saini makubaliano ya mashirikiano
baina ya serikali ya Tanzania na nchi ya Uholanzi katika Nyanja za
maendeleo ya ufugaji wa Samaki na Kuku
Naibu waziri wa Mifugo na Uvuvi
Abdallah Ulega
Ulega pamoja na
Naibu Waziri wa Kilimo maliasili na Usalama wa Chakula Bi
Marjolyn Sonnema
kutoka nchini Uholanzi wakibadilishana nyaraka mara baada ya kutia saini.
Naibu waziri wa Mifugo na Uvuvi
Abdallah Ulega
Ulegaakiongea na waandishi wa habari mara baada ya kutia saini nyaraka hizo za makuliano
mashirikiano
baina ya serikali ya Tanzania na nchi ya Uholanzi katika Nyanja za
maendeleo ya ufugaji wa Samaki na Kuku
Naibu Waziri wa Kilimo maliasili na Usalama wa Chakula Bi
Marjolyn Sonnema
kutoka nchini Uholanzi akimkabidhi
Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo na Mifugo, Elisante Ole Gabriel
zawadi ambayo wametoka nayo nchini uholanzi.
Na Woinde Shizza Michuzi Tv,Arusha
Tanzania ina Upungufu wa Tani zipatazo 350,000 za Samaki kwa
mwaka huku mahitaji yakiwa ni Tani 700,000 ambapo kwa mwaka kiasi cha
tani 350,000 kinazalishwa,hivyo watanzania wametakiwa kuchangamkia
fursa ya uzalishaji ili kufikia malengo ya mahitaji ya samaki.
Kauli
hiyo imeelezwa jijini Arusha na Naibu waziri wa Mifugo na Uvuvi
Abdallah Ulega wakati wa kutiliana saini makubaliano ya mashirikiano
baina ya serikali ya Tanzania na nchi ya Uholanzi katika Nyanja za
maendeleo ya ufugaji wa Samaki na Kuku.
Ulega
amesema kuwa ushirikiano huo wa kimaendeleo na nchi ya Uholanzi
umefikia miaka zaidi ya 40 katika njanja mbali mbali,ikiwemo kilimo cha
Mboga mboga,Viazi Mviringo, Ufugaji wa kuku na Samaki yanayosaidia
kuongeza uzalishaji wa protini na mapato kwa Taifa kwa ujumla.
Amesema
kuwa Tanzania inauhitaji mkubwa wa protini inayotokana na samaki na
kuku ndio maana wamekubaliana na Taifa hilo la uholanzi kuweza kuboresha
Nyanja hizo kwa lengo la kutoa elimu kwa wafugaji na wakulima wa mazao
ya samaki.
“Kama
nchi tumejipanga kuhakikisha ukuaji wa sekta ya ufugaji wa Samaki na
kuku unakuwa kwa kiasi kikubwa kuongeza Pato la taifa kutoka asilimia 9
tunazochangia katika pato la taifa”
Amesema
serikali itaendelea kushirikiana na sekta binafsi katika kuhakikisha
kwamba Uzalishaji wa kuku na Ufugaji wa samaki unaboreshwa na kuona
viwanda vya kuchakata mazao hayo kuondoa changamoto mbali mbali ili
kufikia malengo ya uzalishaji na kuondoa upungufu wa uhitaji wa soko.
Kwa
Upande wake Naibu Waziri wa Kilimo maliasili na Usalama wa Chakula Bi
Marjolyn Sonnema amesema kuwa Ushirikiano huo utasaidia kuboresha sekta
ya ufugaji wa Samaki na kuku na kuinua vipato vya wafugaji wa samaki na
kuku hususani katika sekta binafsi na jamii kwa ujumla.
Amesema
kuwa vile vile uboreshaji huo wa uzalishaji wa kuku na samaki utafanywa
zaidi na sekta binafsi kwa kuwapa uwezo ili kuongeza uzalishaji na
mapato kuongeza mnyororo wa thamani wa uazalishaji wa mazao hayo kwa
wafugaji wa ukanda wa kaskazini.
Post A Comment: