Wednesday, 23 May 2018

UNAI EMERY ATANGAZWA KOCHA MPYA ARSENAL


Kocha mpya wa Arsenal, Unai Emery.

USIKU wa kuamkia leo Arsenal imemtangaza rasmi kocha Unai Emery, kama kocha mkuu badala ya Mikel Arteta. Ilikuwa inafahamika kuwa Arteta ndiye alikuwa na nafasi kubwa ya kuwa kocha mkuu wa timu hiyo, akiridhi nafasi ya Arsene Wenger ambaye amekaa kwenye timu hiyo kwa miaka 22.
Hata hivyo, upepo ulibadilika juzi na sasa kocha huyo ambaye ameipa PSG makombe yote ya ndani msimu uliopita lakini mwishoni mwa msimu akatimuliwa.

Taarifa zinasema kuwa kocha huyo aliulizwa juzi kama yupo tayari kukaa kwenye kiti cha Wenger akasema yupo tayari na uongozi wa timu hiyo ukabadilisha mawazo ghafla juu ya kumpa timu hiyo Arteta ambaye ni kocha msaidizi kwenye kikosi cha Manchester  C i t y

No comments:

Post a comment