UVCCM Dar kuanzisha mfumo mpya wa kanzidata

Umoja wa vijana (UVCCM)  Mkoa wa Dar es Salaam,  imeandaa mfumo wa mpya  wa Kanzidata (Databases) utakaosaidia kuwatambua vijana wa ummoja huo na kupata taarizao.

Akizungumza katika hafla fupi ya kukabidhi kompyuta mapakato(Laptop) 20 zitakazo saidia kuanzishwa kwa mfumo huo Akizungumza leo hii jijini Dar es salaam Mwenyekiti wa Baraza Kuu taifa UVCCM wa Mkoa wa Dar es salaam Gwantwa Alex Mwakijungu , amesema kuwa kuanza kwa mfumo huo utasaidia Sana Jumuiya ya  vijana wa UVCCM mkoa wa Dar es Salaam, kutunza kumbukumbu zake.

"Mimi nime amua kutoa hizi kompyuta ili ziweze kusaidia kuanza kwa mfumo huu  kama alivyoshauri Mwekiti CCM Taifa Dr John Pombe Joseph Magufuli kuwa vijana tuwe wabunifu na kusaidia chama naamka ni hiki nilichukua kitoa kitasaidia kwa kiasi fulani" Alisema Gwantwa” Alisema Mwakijungu.

Naye Katibu wa uhamasishaji na chipukizi mkoa wa Dar es Salaam, Saady khimji amemshukuru Mjumbe huyo  kwa msaada huo na kusema kuwa msaada huo umekuja wakati mwafaka unapokuwa anzishwa mfumo  mpya na ametoa tahadhali kwa vijana wa mkoa wa Dar es Salaam kutoshiriki maandamano haramu yanayo andaliwa katika mitandao ya kijamii.

Adelard Kiliba kutoka kampuni  GPITG (LTD ) ambaye ni mtaalamu wa mfumo huo amesema Mfumo huo utajulikana kama  UVCCM DATABASE SYSTEAM  (DAUDAS) utasaidia pia kuweka kumbukumbu ya nguvu kazi na lasilimali watu,na utakuwa na mfumo wa kihasibu na Wanachama watafanya malipo ya Ada yatafanyika humo humo na unatarajiwa kuanza kutumika April mwaka huu.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa UVCCM Ilala Hamad Pazi, Amesema sasa katika mkoa wa Dar es Salaam hakutakuwa na utata tena wakati wa Uchaguzi na hakutakuwa na watu watakao gushing umri kwa kutaka nafasi za madaraka maana mfumo huu  hautaruhusu hayo.
Previous Post
Next Post

post written by:

0 comments: