Articles by "MAKETE"
Showing posts with label MAKETE. Show all posts

Mkurugenzi Mtendaji wa Mpango wa Kunusuru Kaya Masikini nchini Tanzania, TASAF, Ndg. Sherdac Mziray, leo October 2, 2024 ametembelea na kukagua mradi wa wa Ujenzi wa kituo cha Afya cha Kata ya Kipagalo, kilichopo Wilaya ya Makete, pamoja na Ujenzi wa Bwalo la Chakula katika shule ya Sekondari Lupalilo iliyopo kata ya Tandala, wilayani humo.

Akiwa katika Ukaguzi huo, Ndg. Mziray, amepongeza juhudi za Halmashauri ya Wilaya ya Makete, chini ya Mkurugenzi wake, Ndg. William M. Makufwe kwa namna bora ambayo imekuwa ikisiamamia utekelezaji wa miradi hiyo TASAF, nakuahidi kushirikiana na ofisi hiyo endapo watapata changamoto yeyote.

Aidha, Mziray amesema kuwa, licha ya kuwepo kwa changamoto za kimiundombinu pamoja na upatikanaji wa wazabuni, lakini bado halmashauri imefanikiwa kwa kiasi kikubwa, kukamilisha kwa baadhi ya miradi licha kuwepo kwa mingine inayoendelea kutekelezwa, kama vile Ujenzi wa kituo cha Afya Kipagalo.

Kwa Upande wake, Mkurugenzi wa Fedha, TASAF, Ndg. Godwin Mkisi, ameagiza kamati za usimamizi wa miradi ngazi ya Jamii, CMS kuhakikisha, wanaendelea kuwa na ushirikiano huo huo waliouonesha katika utekelezaji wa miradi ya TASAF ili iweze kukamilika mapema kabla ya mvua kuanza.

Naye, Meneja Miradi na  Ajira za Muda na Miundombinu, TASAF, Ndg. Paul Kijazi, amesema kuwa mwezi wa kumi mwishoni, watafanya ziara ya ukaguzi wa mradi wa kituo cha Afya cha Kipagalo kujiridhisha kama umekamilika kwa majengo ya Matatu ya nyumba za watumishi 2 kwa 1, Jengo la mama na Mtoto pamoja na Jengo la matibabu ya nje OPD ili fedha za awamu ya pili ziweze kutolewa.

Sambamba na hayo, Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Makete, Ngd. William M. Makufwe, amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Sukuhu Hassan, kwa kuendelea kuipa fedha za miradi Halmashauri hiyo, na kwamba wao wataendelea kuisimamia kikamilifu ili iweze kuwa mkombozi kwa wakazi wa wilaya ya Makete.

Akishukuru kwa niaba ya Wananchi, Diwani wa Kata ya Kipagalo, Mhe. Nehemia Sanga, amemshukuru Rais wa Tanzania kwa kuendelea kuipa fedha za kutosha Kata hiyo, kupitia Miradi mbalimbali.

















Wananchi waishio Dar es Salaam, ambao ni wazaliwa wa Wilaya ya Makete, jana Juni 30,2024, wamepata Fursa ya kusomewa taarifa ya Utekelezaji wa Miradi mbalimbali ya Maendeleo ambayo imekuwa ikifanyika katika Wilaya hiyo.

Akisoma taarifa hiyo, Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Makete, Ndg. William M. Makufwe, amesema kuwa Serikali imeboresha Miundombinu ya Elimu , Afya, Usafiri na Maji ili kuhakikisha Jamii inapata huduma iliyo bora, tofauti na ilivyokuwa hapo awali.  

Aidha, Ndg. Makufwe amebainisha kuwa, Serikali imeongeza Bajeti ya Maendeleo katika Wilayani hiyo kutoka Bilioni 26 hadi 36, Ili kuhakikisha kuwa Wilaya hiyo, inaboreshwa katika utolewaji wa huduma za kijamii pamoja na kunyanyua uchumi wa Wilaya hiyo.

Sambamba na hayo, Mkurugenzi Mtendaji wa Wilaya ya  Makete, amewaomba wanamakete kuchangia Maendeleo Wilayani humo, kutokana na kuwepo fursa nyingi za kiuchumi zilizopo katika Wilaya hiyo, katika Kilim, Uvuvi, na Viwanda.

Kwa Upande wake, katibu Mkuu wa Wizara ya Ardhi, Ndg. Antony Sanga, amewashukuru Wanamakete kwa kutoa michango chanya katika Mkutano huo ambayo Umelenga  kuikuza Makete kiuchumi, pamoja na kuhakikisha kuwa wahitimu wa vyuo vikuu wanatengenezewa uwezo wa kuajiriwa na kujiajiri.

Naye, Mbunge wa Makete, Mhe. Festo Sanga, amewataka Wanamakete kuungana na kuwa kitu kimoja katika kuwekeza Nyumbani, kwakuwa Makete ni Moja  na Tuijenge Pamoja.

Sambamba na hayo, Mwenyekiti wa Chama Cha Maendeleo Wilayani Makete, MDA, Ndg. Clement Sanga, amewataka Wanamakete kuwaheshimu viongozi wa Wilaya ya Makete, pamoja na kushirikiana kiuchumi katika kuikuza Wilaya hiyo.

Akihitimisha Mkutano huo,  Kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Njombe Mhe. Antony Mtaka,  Mkuu wa Wilaya Makete, Mhe. Juma Sweda, amesema kuwa, lazima kuwepo na mwendelezo wa Mikutano kama hiyo ili kuhakikisha kuwa Kila mtu anawajibika pamoja na kuweka maeneo ya Ushirikiano kimaendeleo.