Articles by "MAAFAHANANG"
Showing posts with label MAAFAHANANG. Show all posts

 

P%2B1.JPG
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu nchi (Sera, Bunge na Uratibu) Mhe. Jenista Mhagama akizungumza na wananchi wa kata ya Mohoro mara baada ya kukagua eneo ambalo limeathiriwa kwa mafuriko.
P%2B2.JPG
Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu) Dkt. Jim Yonazi akipanda mtumbwi wakati wa kukagua eneo ambalo limeathiriwa kwa mafuriko hayo.
P%2B3.JPG
Baadhi ya Mawaziri waliofika katika Kata ya Muhoro na kukagua eneo ambalo limeathiriwa kwa mafuriko hayo.
P%2B4.JPG
Baadhi ya Vikosi vya Uokoaji Kutoka Jeshi la zimamoto na Uokoaji waliopo katika kata ya Mohoro kwaajili ya kutoa msaada wa maokozi kwa wakazi walioathirika na mafuriko.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge na Uratibu Mhe. Jenista Mhagama amewahakikishia waathirika wa Mafuriko Wilayani Rufiji Mkoani Pwani kuwa Serikali itagharamia huduma zote za msingi zinapatikana wakati wa kipindi hiki.

Ameyasema hayo tarehe 10 Aprili, 2024 wakati alipoongoza timu ya Mawaziri watano wa kisekta waliofika kushuhudia athari zilizotokana na Mafuriko katika eneo la Muhoro wilaya ya Rufiji Mkoani Pwani ambapo pia ametoa tahadhali kwa Wananchi katika maeneo yao kuhakikisha wanafuata maelekezo ya Wataalam na viongozi ili kuepukana na athari zitakazoweza kutokea wakati wa mvua zinapoendelea.

Waziri Mhagama amesema timu hiyo imefika katika eneo hilo ili kila Waziri  kuhakikisha eneo lake linasimamiwa ipasavyo kwa kutafuta mbinu mbadala za kuhakikisha waathirika hao wanapata huduma zinazostahili.

Aidha waziri Mhagama ametoa wito kwa uongozi wa wilaya ya Rufiji kuhakikisha chakula pamoja na mahitaji yanayopelekwa katika eneo hilo yatumike kwa walengwa na si vinginevyo.

"Kwenye huduma hizi za msingi ni pamoja na chakula, na  leo mmeondoka kwenye nyumba zenu na kitu kidogo cha kuwasaidia siku mbili tatu, mmemsikia Naibu waziri wa kilimo hapa tumeshaamua kwamba ni lazima chakula kiletwe cha kutosha na chakula kingine kiko njiani kitaingia leo na kesho, wito wangu mwingine ni kwa viongozi wa wilaya , chakula hiki kigaiwe kwa wahusika tu na si kunufaisha watu wengine ambao hawahusiki ,nitafuatilia na kuhakimisha kinawafikia waathirika." Alisema Mhagama.

Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Pwani Mhe. Abubakar Kunenge amewataka wananchi kuendelea kuhama na kwenda katika  maeneo ambayo hayajaathirika na maji ili kuweza kupatiwa huduma zinazotolewa na Serikali.

"Tuangalie Maji maana  yanaendelea na mvua zinaongezeka kwa hiyo tuchukue tahadhali kadri maji yanavyoongezeka tusogee ,tusiseme tumezoea maji haya ni mafuriko yametokea mvua zimekuwa nyingi na nyingine sio za hapa lakin zinaingia katika mto yanajaa hapa, kubwa ni kwamba hakuna mtu atakayekufa kwa njaa hakuna atakae kosa huduma ya kiafya wala ya kuhifadhiwa na matibabu maana Serikali inawathamini sana." Alisema Kunenge.

SERIKALI ya nchi ya Qatar imetoa msaada wa vyakula kwa ajili ya waathirika wa maafa ya maporomoko ya tope wilayani Hanang mkoani Manyara.

Akipokea msaada huo  katika Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro (KIA), Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge na Uratibu Mhe. Ummy Nderiananga alisema kuwa, misaada ya kibinadamu iliyotolewa na Qatar ni chakula kikavu katika vifungashio 1440, chakula kilicho tayari kuliwa katika vifungashio 3024 na vifaa vya usafi wa wanawake 4200.

Naibu Waziri huyo alisema kuwa, maporomoko hayo yalisababisha maafa katika Kata nne ambazo ni Gendabi, Ganana, Katesh na Jorodom na kusababisha madhara mbalimbali pamoja na vifo vya watu 89, majeruhi 139, nyumba 261 ziliathirika, mashamba ekari 754 ya wakulima 369 pamoja na Biashara 713.

 “Serikali tunatambua mchango wa wadau wote ikiwemo wananchi, sekta binafsi asasi za kiraia na kidini, mashirika ya kimataifa na Umoja wa mataifa kwa ushiriki wao katika kusaidia wananchi walioathirika katika Wilaya ya Hanang.Pia Serikali kwa kushirikiana na wadau na wananchi imeendelea kuchukua hatua kuhakikisha wananchi wa Hanang walioathirika wanarejea katika hali ya maisha ya awali,”Alisema Mhe. Ummy.

 Naibu Waziri huyo aliongeza kuwa kwa sasa pamoja na kutoa misaada ya kibinadamu Serikali inaendelea na maandalizi ya ujenzi wa nyumba 108 za wananchi ambao nyumba zao zilibomoka kabisa au kuwa katika maeneo hatarishi katika eneo la Waret, Kijiji cha Gidagamond Kata ya Mogitu.

“Msaada huu utaenda kugusa maisha ya wananchi wa Hanang na Serikali inathamini ushiriki wa Wananchi wa Qatar na Serikali yake pamoja na taasisi ya misaada ya Qatar kupitia msaada wa kibinadamu ambao umetoa mchango mkubwa katika kuleta faraja, upendo na matumaini mapya kwa waathirika,”Alishukuru.

Kwa upande wake, Balozi wa nchi ya Qatar nchini Tanzania, Fahad Rashed Almarekhi alibainisha kwamba , Serikali ya Qatar imeamua kutoa msaada kwa Watanzania ambao wamekumbwa na maafa Hanang na utoaji wa msaada huo ni kielelezo cha kuthibitisha ukaribu na uhusiano mzuri uliopo baina ya nchi hizo mbili.

“Ujumbe wetu huu unaonyesha namna tulivyo na mashirikiano mazuri katika Nchi zetu hizi mbili, baada ya msaada huu tuma timu ya wataalam kuja kutambua mahitaji mengine ambayo hayakuguswa na msaada huu ili kutoa msaada mwingine ambao utakuwa ni suluhisho ya wananchi wa Hanang,”Alibainisha Mhe. Balozi Almarekhi.

Aidha Mkuu wa Mkoa wa Manyara Mhe. Queen Sendiga aliahidi kuhakikisha anasimamia vyema ugawaji wa misaada hiyo ili kuwafikia waathirika kama ilivyokusudiwa.

Ikumbukwe mnamo tarehe 03 Disemba, 2023 yalitokea maafa ya maporomoko ya tope yaliyoambatana na mawe, miti, magogo na maji kwa wingi kutoka Mlima Hanang kuelekea makazi ya watu.

Jumuiya ya Kampuni za Kuongoza Uwindaji wa Kitalii Tanzania (Tanzania Hunting Operators Association-TAHOA) imeendelea kutoa mkono wa pole kwa  jamii ya Wana Hanang waliopatwa na maafa ya mafuriko yaliyotokea mwezi Desemba mwaka jana ambapo leo  imekabidhi mabati 1143 ikiwa ni mchango wa vifaa vya ujenzi.

 Mchango huo wa mabati unakuja ikiwa ni mwendelezo wa TAHOA   kutoa mkono wa pole kwa Wana Hanang ambapo awali ilichangisha fedha takribani shilingi za kitanzania milioni 47 na kuzikabidhi kwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu), Mhe. Jenista Mhagama (Mb)

Akizungumza wakati wa makabidhiano hayo leo Januari 11, 2024 Wilayani Hanang Mkoani Manyara Katibu Mkuu wa TAHOA, Suleiman Masato amesema kuwa TAHOA imeguswa na maafa hayo huku ikiahidi kuendelea kutoa michango mbalimbali ili kuwagusa Waathiriwa hao.

“Leo tumekabidhi jumla ya mabati  1143 yenye geji 28 mita 3 ambayo ni kiwango kinachokubalika na Serikali”amesema Masato.

Naye, Mkuu wa Wilaya ya Hanang, Mhe. Janeth Mayanja ameishukuru TAHOA kwa kuguswa na matatizo yaliyotokea Wilayani Hanang na kwa  kuunga mkono juhudi za Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan za kuwajengea makazi bora wananchi wa Hanang.

“Mchango huu mliouleta umegusa maisha ya wananchi wa Hanang waliopata madhara ya mafuriko kama tunavyojua wengine wamepoteza makazi na vifaa mbalimbali na nafahamu mlitanguliza kutoa mchango wa fedha katika akaunti ya maafa lakini leo mmekuja kwa mara nyingine hapa Hanang kwa ajili ya kuleta vifaa vya ujenzi, hivyo kwa niaba ya Serikali nawashukuru sana”amesema Mhe. Mayanja.

Jumuiya ya Kampuni za Kuongoza Uwindaji wa Kitalii Tanzania (Tanzania Hunting Operators Association-TAHOA) imeendelea kutoa mkono wa pole kwa  jamii ya Wana Hanang waliopatwa na maafa ya mafuriko yaliyotokea mwezi Desemba mwaka jana ambapo leo  imekabidhi mabati 1143 ikiwa ni mchango wa vifaa vya ujenzi.

 Mchango huo wa mabati unakuja ikiwa ni mwendelezo wa TAHOA   kutoa mkono wa pole kwa Wana Hanang ambapo awali ilichangisha fedha takribani shilingi za kitanzania milioni 47 na kuzikabidhi kwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu), Mhe. Jenista Mhagama (Mb)

Akizungumza wakati wa makabidhiano hayo leo Januari 11, 2024 Wilayani Hanang Mkoani Manyara Katibu Mkuu wa TAHOA, Suleiman Masato amesema kuwa TAHOA imeguswa na maafa hayo huku ikiahidi kuendelea kutoa michango mbalimbali ili kuwagusa Waathiriwa hao.

“Leo tumekabidhi jumla ya mabati  1143 yenye geji 28 mita 3 ambayo ni kiwango kinachokubalika na Serikali”amesema Masato.

Naye, Mkuu wa Wilaya ya Hanang, Mhe. Janeth Mayanja ameishukuru TAHOA kwa kuguswa na matatizo yaliyotokea Wilayani Hanang na kwa  kuunga mkono juhudi za Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan za kuwajengea makazi bora wananchi wa Hanang.

“Mchango huu mliouleta umegusa maisha ya wananchi wa Hanang waliopata madhara ya mafuriko kama tunavyojua wengine wamepoteza makazi na vifaa mbalimbali na nafahamu mlitanguliza kutoa mchango wa fedha katika akaunti ya maafa lakini leo mmekuja kwa mara nyingine hapa Hanang kwa ajili ya kuleta vifaa vya ujenzi, hivyo kwa niaba ya Serikali nawashukuru sana”amesema Mhe. Mayanja.



Na Munir Shemweta, WANMM HANANG

 

Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Geophrey Mizengo Pinda ametembelea maeneo yaliyoathirika Mafuriko yaliyotokana na maporomoko ya mawe na tope kutoka mlima Hanang.

 

Mhe. Pinda ametembelea maeneo hayo tarehe 20 Desemba 2023 kabla ya kuhudhuria kikao cha Utekelezaji Maagizo kuhusu Mafuriko yaliyotokana na maporomoko ya mawe na tope kutoka mlima Hanang.

 

Naibu Waziri Pinda alitembelea maeneo yaliyoathirika kwenye mji wa Katesh pamoja na kijiji cha Gendabi mkoani Manyara.

 

Akiwa katika maeneo hayo Mhe Pinda alikutana na Waziri wa nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Bunge, Sera na Uratibu) Jenister Mhagama aliyekwenda kutembelea maeneo mbalimbali katika halmashauri ya Hanang kujionea urejeshaji wa hali katika maeneo yaliyoathiriwa na maafa ya maporomoko na tope na mawe mlima Hanang.

 

Wakiwa katika maeneo ya waathirika, Mawaziri walijionea hali halisi ya urejeshaji hali katika maeneo yaliyoathirika na maafa pamoja na kukagua ugawaji misaada kwa wananchi walioathirika na maafa.

 

Baadhi ya Wananchi waliozungumza na Mawaziri hao wameeleza kuridhishwa kwao na juhudi za serikali hasa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt Samia Suluhu Hassan katika kuwasaidia wale waliokumbwa na athari ya mafuriko katika eneo hilo.

 

‘’Tunaomba mtupelekee salamu na shukran zetu kwa Rais Samia kutokana na juhudi zake na jinsi alivyolipa uzito suala hili la waathirika wa mafuriko, tumhakikishie tuko pamoja naye’’ walisema.

 

Mafuriko yaliyotokana na maporomoko ya mawe na tope kutoka mlima Hanang yamesababisha jumla ya wananchi 87 miili yao kupatikana baada ya kupoteza maisha na majeruhi kuendelea kupata matibabu katika hospitali ya Hydom, wilaya na mkoa. Sambamba na hilo baadhi ya wananchi wanaendelea kupata hifadhi katika maeneo ya taasisisi za elimu zilizopo Katesh baada ya makazi yao kuharibiwa.



OR-TAMISEMI 


Naibu Waziri Ofisi ya Rais - TAMISEMI anayeshughulikia Afya Dkt. Festo Dugange amesema idadi majeruhi wa mafuriko ya tope Hanang mkoani Manyara wanaoendelea na matibabu imepungua kutoka 117 hadi 36 na sh.milioni 560 zimetolewa kwaajili ya huduma za afya kwa wathirika hao.

Dkt. Dugange akiwa ameambatana Mhe. Jenista Mhagama Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu – Sera,Bunge na Uratibu  na mhandisi Godfrey Kasekenya Naibu Waziri wa Ujenzi katika ukaguzi wa maeneo yaliyoathirika ambayo serikali inayarejesha kwenye hali yake katika Mji wa Katesh wilaya ya Hanang, amesema;

“Tunauhakika hao 36 waliobahi wataendelea kuruhusiwa kurejea nyumbani kuendelea na majukumu yao na jambo la muhimu kwenye majanga haya serikali inajitahidi kudhibiti magonjwa ya mlipuko kujitokeza na sehemu kama hii tulichokifanya tumeimasha mfumo ya udhibiti wa magonjwa ya mlipuko kwenye jamii yetu na katika kambi zetu” Dkt. Dugange

Naye Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera,Bunge na Uratibu) Mhe. Jenista Mhagama amesema serikali imeanza mazungumzo na taasisi za kifedha ili kutoa unafuu kwa wafanyabiashara walioathiriwa na mafuriko  na ameendelea kushukru wadau wanaoendelea kutoa msaada.

Waziri Jenista Mhagama amesema kuwa mbali na Serikali kurejesha miundombinu pia imeendelea kuwa bega kwa bega na Wananchi sambamba na kutoa maagizo kwa Wataalamu wa Satellite kuanza kuangalia Kaya zote na kuona zipi zimeathirika zaidi huku ikiendelea kutoa msaada zaidi. 

Aidha,Naibu Waziri wa Ujenzi, Eng. Godfrey Kasekenya amesema hadi sasa urejeshaji wa miundombinu ya barabara na makalvati yaliyoharibiwa na maporomoko ya tope na mawe yaliyotokea Desemba 3, 2023 kwenye Mji wa Katesh wilayani Hanang mkoani Manyara umefikia asilimia 75. 

Kasekenya amesema kazi hiyo kukagua imefanywa na  Wakala ya Barabara (TANROADS) wakishirikiana na Wakala ya Barabara za  Vijijini na Mijini (TARURA). 


Meneja Uhusianoo wa Umma wa Amsons Gruop Bhoke Rioba(kulia) akikabidhi hundi ya Sh.milioni 100 kwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge na Uratibu Jenista Mhagama (wa pili kushoto)kwa ajili ya mfuko wa maafa kusaidia waathirika wa mafuriko ya matope yaliyotokea Hanang mkoani Manyara.Kulia ni Naibu Waziri wa Afya Dk.Mollel


 KAMPUNI ya Amsons Group kupitia kampuni zake za Camel Oil na Camel Cement zimekabidhi hundi ya Sh.milioni 100 kwa Serikali kwa ajili ya kusaidia waathirika wa mafuriko ya matope yaliyotokea Hanang mkoani Manyara.


Mbali na kukabidhi hundi hiyo pia Kampuni ya Camel Oil imetoa misaada mbalimbali kama Magodoro, maji na mablanketi kwa ajili ya waathirika hao na hiyo ni sehemu ya kampuni kurejesha tabasamu kwa wananchi waliokumbwa na mafuriko hayo yaliyosababisha vifo, majeruhi na uharibifu wa mali.

Akizungumza baada ya kukabidhiwa hundi ya milioni 100 pamoja na mahitaji hayo, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge na Uratibu Jenista Mhagama ameishukuru kampuni hiyo kwa kutoa fedha na msaada huo vifaa hivyo kwa ajili ya waathirika wa mafuriko hayo.

"Tumepokea Sh.milioni 100 kutoka Camel Cement lakini na vitu vingine kutoka Camel Oil na tunaomba kwa niaba ya Serikali mtupelekee salamu kwa menejiment tunashukuru.

"Bado tunahitaji misaada ya kibinadamu ili kuwezesha ufumbuzi wa muda na wa kudumu kwa ajili ya ndugu zetu ili maisha yarejee kama kawaida " amesema Waziri Jenista.

Awali wakati abakabidhi misaada hiyo Meneja Masoko na Uhusiano wa Umma wa Amsons Group, Bhoke Rioba amesema Camel Cement imeweka fedha kwenye akaunti ya maafa ya Serikali kiasi cha Sh.milioni 100, magodoro 100 pamoja na mashuka 100.

Amesema kutoa kwao fedha na msaada huo ni muendelezo wa kampuni hizo kwenye kampeni yake ya kurudisha tabasamu kwa jamii ya Tanzania.


Na. WAF - Hanang, Manyara 


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan ametoa wito kwa wananchi Mji mdogo wa Katesh Wilaya ya Hanang Mkoani Manyara na Watanzania kwa ujumla kuendelea kuchukua tahadhari za magonjwa ya mlipuko kwa kuchukua hatua za matumizi ya maji safi na salama.

Dkt. Samia ametoa wito huo leo Disemba 7 ,2023 wakati akizungumza na wananchi  mji mdogo wa Katesh Wilayani Hanang Mkoa Manyara baada ya Disemba 3, 2023 kukumbwa na maafa ya mafuriko yaliyosababisha maporomoko ya udongo kutoka mlima Katesh na kusababisha madhara makubwa ikiwemo majeruhi,vifo na upotevu wa mali.

"Jambo kama hili linapotokea huwa yanatokea magonjwa ya mlipuko ,niwaombe wananchi wachukue hatua stahiki za kuzingatia kanuni za afya pindi wanapotumia maji wazingatie kuepuka magonjwa ya mlipuko ikiwemo kuhara "amesema.

Aidha, Rais Samia ametoa maagizo kwa Wizara ya Afya kuhakikisha elimu na ufuatiliaji kwa kina inatolewa kwa wananchi.

"Wizara ya Afya hakikisheni elimu juu ya kujikinga na madhara yanayoweza kutokea kutokana na mafuriko inatolewa pia kufuatilia kwa kina majeruhi mpaka kuhakikisha wanakuwa katika hali ya kawaida"amesema Dkt Samia.

Halikadhalika, Dkt.Samia ameagiza kuhakikisha msaada wa Kisaikolojia unaendelea kutolewa pamoja na huduma za maji safi na salama kuendelea kuimarishwa.

Hata hivyo,ametumia fursa hiyo kuwashukuru wadau kwa kutoa msaada ambapo jumla ya Tsh.Bilioni 2.5 zimetolewa na wadau kutoka nje ya nchi huku akielekeza zitumike kujenga makazi ya kudumu kwa waathiriwa.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan amewasili katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro tarehe 7 Desemba, 2023 tayari kuelekea Katesh wilayani Hanang kulipotokea maafa ya mafuriko makubwa.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan amewasili katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro tarehe 7 Desemba, 2023 tayari kuelekea Katesh wilayani Hanang kulipotokea maafa ya mafuriko makubwa. 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan amewasili katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro tarehe 7 Desemba, 2023 tayari kuelekea Katesh wilayani Hanang kulipotokea maafa ya mafuriko makubwa. 




Na John Walter-Manyara

Zoezi la kurejesha mji wa Katesh katika hali yake ya awali ili kuwezesha shughuli za uzalishaji kuendelea, imefikia katika hatua nzuri ambapo asubuhi ya leo tarehe 07 Disemba 2023 Maduka na huduma nyingine zimeanza kurejea katika hali ya kawaida.

Waziri wa Ujenzi, Innocent Bashungwa akishirikiana na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu), Jenista J. Mhagama pamoja na viongozi wengine wameendelea kupiga kambi ya kusimamia uzoaji wa tope usiku na mchana ikiwa ni pamoja na kusafisha mji wa Katesh wilayani Hanang.

 


Waziri wa Ujenzi, Innocent Bashungwa amesema kazi ya kuondoa tope inaendelea na shughuli kubwa inayofanyika kwa sasa ni kufungua mitaa yote ya mji wa Katesh na kurejesha mji katika hali yake ya awali kwa kuwezesha shughuli za uzalishaji kuendelea.

Ameyasema hayo mapema asubuhi hii wakati wakikagua kazi zilizofanyika ambapo aliambatana na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu), Jenista J. Mhagama, Waziri wa Madini, Antony Mavunde na Viongozi wengine , leo tarehe 6 Disemba 2023.

“Maelekezo ya Mheshimiwa Rais, Dkt. Samia Suluhu Hassan ni kuhakikisha leo kufikia usiku, mji wa Katesh na mitaa yake iwe imesafishwa ili kushughuli za uzalishaji ziendelee kama mnavyoona Wafanyabiasha wameanza kufungua Maduka” amesema Bashungwa

Bashungwa amesema TANROADS kwa kushirikiana na TARURA tayari ameweka mpango kazi wa pamoja ambao  utahakikisha kazi hiyo inaendelea kufanyika usiku na mchana mpaka shughuli hiyo itakapokamilika.

Aidha, Waziri Bashungwa amevipongeza Vyombo vya  ulinzi na Usalama, kwa kazi kubwa wanayofanya  ambapo wamehakikisha wanaleta vijana wa JKT wanaoshiriki katika zoezi la uokozi ikiwa ni pamoja na kusaidia kazi za kurejesha hali nzuri katika mji wa Katesh.

Naye, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu), Jenista Mhagama amesema kuwa wanaendelelea kutekeleza maagizo ya Mheshimiwa Rais ambayo jambo la kwanza lilikuwa ni kukabiliana na mafuriko na kuhakikisha matibabu kwa wahanga yanatolewa bure. 

Amesema jambo jingine ni kuhakikisha wanaendelea kutafuta miili, kazi ambayo inaendelea na inafanywa na vikosi vya ulinzi na usalama na kuhakikisha wale ambao wanaokolewa wanatayarishiwa maeneo ya kuishi na kupatiwa huduma nyingine za kijamii. 

Vilevile , Waziri Jenista ameongeza kuwa, Serikali inaendelea kupokea michango kutoka sehemu tofauti tofauti kwa ajili ya waanga wa maafa ili kuweza kuwarudisha katika hali yao ya awali.

Kazi hiyo ya kuondoa tope katika Mji wa Katesh Wilaya ya Hanang’ Mkoa wa Manyara na kurejea  katika hali yake ya awali ni baada ya kuharibiwa na maporomoko ya matope kutoka Mlima Hanang’ na kusababisha madhara ikiwemo vifo, majeruhi na uharibifu wa mali na miundombinu.



Na John Walter-Manyara

Serikali imesema jumla ya idadi ya wagonjwa waliolazwa katika hospitali mbalimbali kutokana mafuriko na maporomoko ya maji Katesh na Gendabi wilayani Hanang' Mkoani Manyara imefika 93.

Awali mkuu wa mkoa wa Manyara Queen Sendiga alitangaza kuwa Majeruhi walikuwa ni 85 hadi Jana jioni.

Mganga mkuu wa Serikali Profesa Tumaini Nagu amesema majeruhi 11 waliolazwa katika hospitali ya rufaa ya mkoa wa Manyara, watano ni Watoto ambapo wawili wapo kwenye uangalizi maalum, wawili wamefanyiwa upasuaji wa kuondolewa bandama kutokana na majeraha waliyoyapata, watatu watatu wamefanyiwa upasuaji Mdogo wa mifupa na kuwekwa mifupa vizuri kwa kuwa walipata mvunjiko.

Serikali imewaongezea nguvu Madaktari Hospitali ya rufaa mkoa wa Manyara kwa kuwapatia Madaktari 10 kutoka hospital ya Rufaa ya mkoa wa Dodoma na wengine 12 wa hospitali ya rufaa ya mkoa wa Arusha na Singida.

Katibu Mkuu wizara ya Afya Dkt.John Jingu amesema tangu janga lililotokea Desemba 3,2023, wizara imeendelea kujipanga kuwahudumia kikamilifu majeruhi wote.

Naibu Waziri wa Afya Dkt. Godwin Mollel amesema kila kitu kinakwenda sawa kama alivyoelekeza Rais Samia Suluhu Hassan.




 Na John Walter ; Hanang'

SERIKALI kupitia Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge na Uratibu imechukua hatua za haraka kwa wahanga wa maafa yaliyosababishwa na maporomoko ya tope yaliyotokea tarehe 03 Disemba, 2023 ambapo yalitoka mlima Hanang uliopo Mkoa wa Manyara na kusababisha vifo vya watu, majeruhi na uharibifu mkubwa wa miundombinu mbalimbali yakiwemo mashamba, na makazi ya wananchi wa eneo hilo.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia masuala ya Sera, Bunge na Uratibu Mhe. Jenista Mhagama, Waziri wa Ujenzi Mhe. Innocent Bashungwa, Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu), Dkt. Jim Yonazi pamoja na Wakuu wa Vyombo vya Ulinzi na Usalama wamefika katika kijiji cha Gendabi kata ya Gendabi Wilaya ya Hanang’ mkoani Manyara eneo yalipotokea maporomoko ya tope Leo tarehe 04 Disemba 2023.

Viongozi hao wameongozwa na Mkuu wa Mkoa Manyara Mhe. Queen Sendiga kufika katika Kijiji cha Gendabi ambalo ni eneo liliothirika Maporomoko ya tope kutoka Mlima wa Hanang yaliyotokea usiku wa kuamkia tarehe 03 Disemba 2023.

Akiwa eneo la tukio hilo, Waziri Mhagama, amewaomba wananchi hao kupokea pole ambazo zinatoka kwa Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania ambaye aliagiza lazima KUfika eneo la tukio na kuona nini kifanyike kwa dharura kuhusu uokoaji pamoja na makazi kwa waathirika hao.

“Mambo haya yakitokea kuna mambo ya haraka yanatakiwa yafanyike kwa dharura hivyo tumekuja na kushauriana namna ya kujipanga kwa pamoja ili kufanikisha jambo hilo kwa uharaka”. Ameongeza Mhagama

Ameongeza kuwa, maelekezo ya Mheshimiwa Rais kwanza kuona namna gani wanaweza kuendelea kuokoa watu na kazi hiyo wanaendelea nayo vikosi vya uokoaji, pia kuangalia namna gani ya kuweza kuwasitiri wenzetu waliotangulia mbele ya haki.

Aidha, Waziri Mhagama amesema kuwa Serikali imeshaleta wataalamu wa Miamba watatoa taarifa ya nini kilichotokea na nini kifanyike katika mlima wa Hanang.

Kwa upande wake Waziri wa Ujenzi, Innocent Bashungwa amesema kazi ya kufungua miundombinu ya barabara inaendelea ili kurahisia kazi za uokoaji na kufikisha huduma muhimu za kijamii katika meneo yaliyoathirika.

Amesema Wakala wa Barabara nchini (TANROADS) tayari wamefungua Barabara ya Singida-Babati ambayo awali ilikuwa haipitiki kutokana na kujaa tope na magogo ya miti kutoka milimani.
Naye Mbunge wa Hanang’ Mhe. Samwel Hayuma aliipongeza serikali kwa namna inavyoendelea kuchukua hatua za haraka za kuokoa na kusaidia wahanga wa maafa hayo, huku akiwasisitiza wananchi hao kuendelea kuchukua tahadhari kwa maeneo yote yaliyoathirika na tope hilo.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu) Mhe. Jenista J. Mhagama, Waziri wa Ujenzi Innocent Bashungwa, pamoja na Wakuu wa Vyombo vya ulinzi na Usalama wamefika katika kijiji cha Gendabi kata ya Gendambi Wilaya ya Hanang mkoani Manyara eneo yalipotokea mafuriko ambayo yamesababisha vifo vya watu, majeruhi na uharibifu mkubwa wa Miundombinu mbalimbali, yakiwamo mashamba na makazi ya wananchi, Leo tarehe 04 Disemba 2023

Viongozi hao wameongozwa na Mkuu wa Mkoa Manyara, Queen Sendiga kufika katika Kijiji cha Gendabi ambalo ni  eneo lililoathirika sana na Maporomoko ya Matope kutoka Mlima wa Hanang yaliyotokea usiku wa kuamkia tarehe 03 Disemba 2023.

Akiwa eneo la tukio hilo, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu) Mhe. Jenista J. Mhagama, amewaomba wananchi hao kupokea pole ambazo zinatoka kwa Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania ambaye aliagiza lazima kufika  eneo la tukio na kuona  nini kifanyike kwa dharura kuhusu uokoaji pamoja na makazi kwa waathirika hao.

 "Mambo haya yakitokea  kuna mambo ya haraka  yanatakiwa yafanyike kwa dharura hivyo tumekuja na kushauriana namna ya kujipanga kwa pamoja ili kufanikisha jambo hilo kwa uharaka”. Ameongeza Mhagama

ameongeza kuwa, maelekezo ya Mheshimiwa Rais kwanza kuona namna gani tunaweza kuendelea kuokoa watu na kazi hiyo wanaendelea nayo vikosi vya uokoaji, pia kuangalia namna gani ya kuweza kuwasitiri wenzetu waliotangulia mbele ya haki.

Aidha, Waziri Mhagama amesema kuwa Serikali imeshaleta wataalamu wa Miamba watatoa taarifa ya nini kilichotokea na nini kidanyike katika mlima wa Hanang

Kwa upande wake Waziri wa Ujenzi, Innocent Bashungwa amesema kazi ya kufungua miundombinu ya barabara inaendelea ili kurahisia kazi za uokoaji na kufikisha huduma muhimu za kijamii katika meneo yaliyoathirika.

Amesema Wakala wa Barabara nchini ( TANROADS) tayari wamefingua Barabara ya Singida-Babati ambayo awali ilikuwa haipitiki kutokana na kujaa tope na magogo ya miti kutoka milimani.