Ujenzi wa jengo la VIWANGO HOUSE Mwanza la Shirika la Viwango Tanzania(TBS) ni sehemu ya jitihada za Serikali ya Awamu ya Sita chini ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan za kuboresha miundombinu ya utoaji huduma na kuchangia utekelezaji wa malengo ya Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050.

Akizungumza wakati wa ziara ya Bodi ya Wakurugenzi wa Shirika la Viwango Tanzania (TBS) ya kukagua maendeleo ya mradi huo, Mwenyekiti wa Bodi, Prof. Othman Chande Othman amesema jengo hilo linalenga kusogeza huduma za viwango karibu na wananchi na wafanyabiashara wa Kanda ya Ziwa.

Kwa upande wake, Mkurugenzi Mkuu wa TBS, Dkt. Ashura Katunzi, amesema jengo hilo linatarajiwa kukamilika mwishoni mwa mwaka 2026 na kuongeza ufanisi katika utoaji wa huduma kwa sekta ya viwanda na biashara.

Ameongeza kuwa eneo la kimkakati la jengo hilo litasaidia pia kurahisisha upatikanaji wa huduma kwa wafanyabiashara wanaohudumia masoko ya nchi jirani za Rwanda, Burundi na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC).

Naye Mshauri Elekezi wa Mradi, Chris Olomi, amesema ujenzi umefikia asilimia 95.2, huku gharama ya mradi ikiwa shilingi bilioni 12.

Kukamilika kwa VIWANGO HOUSE Mwanza kunatarajiwa kuimarisha huduma za TBS, kusaidia ukuaji wa viwanda na biashara na kusogeza huduma bora karibu zaidi na wananchi.
Share To:
Next
This is the most recent post.
Previous
Older Post

OSCAR ASSENGA

Post A Comment: