Serikali ya Tanzania imefanya mazungumzo na Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) kuhusu kuharakisha maandalizi na utekelezaji wa Mradi wa Ustahimilivu wa Ukanda wa Pwani, kufuatia kuidhinishwa kwa andiko la awali la mradi lililowasilishwa na NEMC mwezi Juni 2024.
Mradi huu unalenga kulinda mifumo ikolojia ya bahari na pwani, ikiwemo mikoko, miamba ya matumbawe na nyasi bahari, pamoja na kuimarisha ustahimilivu wa jamii na uchumi wa pwani Tanzania Bara na Zanzibar.
Tanzania imependekeza kuandaliwa kwa mpango wa pamoja wa siku 90 kati ya AfDB na NEMC ili kuharakisha maandalizi ya mradi na upatikanaji wa fedha kwa ajili ya utekelezaji.
Dhamira yetu ni kubadili ahadi za kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi kuwa vitendo vinavyolinda mazingira, jamii na Uchumi wa Buluu.
#NEMC #AfDB #Tanzania #UstahimilivuWaPwani #MabadilikoYaTabianchi #UchumiWaBuluu







Post A Comment: