- Yazindua Kiwanda, chenye uwezo wa kuzalisha tani 28 kwa saa

-Yatoa Toyo 40 kuleta ajira kwa waendeshaji wake

📍Dodoma

SHIRIKA la Madini la Taifa (STAMICO) limetekeleza azma yake ya kuwa lango la kukuza uchumi kupitia rasilimali madini kwa kuzindua kiwanda kikubwa na cha kisasa cha kuzalisha nishati safi na salama ya kupikia ya Rafiki Briquettes jijini Dodoma.

Uzinduzi wa kiwanda hicho uliofanyika Novemba 7, 2026, katika Kata ya Chigongwe, jijini Dodoma, umefanywa na Waziri wa Madini, Mhe. Anthony Mavunde, ambaye alikuwa mgeni rasmi katika hafla hiyo.

Akizungumza katika hafla hiyo, Mkurugenzi Mkuu wa STAMICO, Dkt. Venance Mwasse amesema, hatua hiyo inayolenga kuongeza upatikanaji wa nishati hiyo, kukuza viwanda vya ndani na kuimarisha mchango wa sekta ya madini katika maendeleo ya taifa.

Amesema kuwa moja ya manufaa makubwa ya uwekezaji huo ni kukuza viwanda vya ndani kupitia teknolojia ya uongezaji thamani wa madini na matumizi ya rasilimali zilizopo nchini ukifungua fursa za uwekezaji na biashara.

Amesema kiwanda hiki kinaenda kuleta mabadiliko ya kiuchumi kwa jamii ya Chigongwe kupitia utoaji wa huduma mbalimbali zitakazotolewa kwa wendesha kiwanda hicho ikiwemo mahitaji ya kila siku na uuzaji wa vipuli

Ameongeza kuwa kiwanda kinaenda kutoa ajira kwa Watanzania kuanzia kwenye uzalishaji hadi usambazaji wa nishati hiyo ya Rafiki Briquettes.

Amesema kiwanda hicho kimegharimu Sh bilioni 3.70, huku uwekezaji wa jumla wa miundombinu na vifaa vilivyozinduliwa katika hafla hiyo ukifikia Sh bilioni 6.09, ikiwa ni sehemu ya mkakati wa STAMICO wa kuongeza thamani ya rasilimali za madini na kuimarisha uzalishaji wa bidhaa zinazowanufaisha Watanzania.

Dkt. Mwasse amesema STAMICO imeendelea kutekeleza mageuzi kupitia mkakati wa MASTASHA (Make STAMICO Shine Again), unaolenga kuifanya kampuni hiyo kuwa miongoni mwa mashirika yenye ufanisi na uwezo wa ushindani katika sekta ya madini.

Amefafanua kuwa vifaa hivyo vitasaidia kuwawezesha mawakala na wajasiriamali, wakiwemo wanawake na vijana, kushiriki katika biashara ya usambazaji wa nishati safi ya kupikia na hivyo kujipatia kipato.

Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya STAMICO ambaye pia ni Mkuu wa Mkoa wa Kigoma, Mhe. Simon Sirro, amesema uzinduzi wa kiwanda hicho ni matokeo ya mikakati na ushirikiano kati ya bodi na menejimenti ya shirika katika kuhakikisha STAMICO inaendelea kuimarika na kutekeleza majukumu yake kwa ufanisi.

Amesema bodi itaendelea kusimamia utekelezaji wa mikataba na mipango ya shirika ili kuhakikisha uwekezaji unaofanyika unaleta tija kwa taifa na kuunga mkono juhudi za Serikali ya Awamu ya Sita chini ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan katika kuimarisha matumizi ya nishati safi ya kupikia.

Mhe. Sirro ametoa wito kwa wananchi wa Dodoma na Watanzania kwa ujumla kutumia nishati safi ya Rafiki Briquettes, akisisitiza kuwa ushiriki wa wananchi ni muhimu katika kufanikisha malengo ya Serikali ya kupunguza matumizi ya nishati chafu.

Aidha, ameiomba STAMICO kuimarisha mikakati ya kujitangaza na kupanua masoko ya bidhaa hiyo, huku akizitaka taasisi za umma, hususan shule na magereza, kuanza kutumia Rafiki Briquettes ili kuongeza mahitaji na kusaidia upanuzi wa uzalishaji.

Uzinduzi wa kiwanda hicho ni sehemu ya juhudi za STAMICO za kuongeza thamani ya rasilimali za madini nchini, kukuza viwanda vya ndani na

Kiwanda hicho ni cha nne cha Rafiki Briquettes kuzinduliwa nchini, kikiwa na uwezo wa kuzalisha tani 20 za nishati safi ya kupikia kwa saa ili kuchangia utekelezaji wa dhamira ya taifa ya kuhakikisha nishati safi ya kupikia inapatikana kwa wananchi kwa gharama nafuu na kwa uhakika.
Share To:
Next
This is the most recent post.
Previous
Older Post

OSCAR ASSENGA

Post A Comment: