📌 Asema ziara ya Makamu wa Rais Mbinga kufungua fursa za viwanda na miundombinu Nyanda za juu kusini;
📌 Wizara kupitia WRRB kushiriki kusimamia utekelezaji wa mfumo huo kuwezesha bei shindani Kwa wakulima na mauzo Nje ya nchi.
📌Ahimiza wananchi wa Mbinga kujitokeza Kwa wingi ziara ya Makamu wa Rais.
Waziri wa Viwanda na Biashara ambae pia ni Mbunge wa jimbo la Mbinga vijijini Mhe. Judith Kapinga, amesema Mfumo wa Stakabadhi za Ghala ni muhimu katika kuongeza thamani ya mazao, kuwawezesha wakulima kupata bei shindani na kulinda maslahi yao katika biashara ya mazao nchini.
Mhe. Kapinga ameeleza hayo leo, Novemba 9, 2026, katika mahojiano maalumu na kituo cha redio cha Ruvuma FM, akizungumzia masuala yanayohusu ziara ya kikazi ya Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Deogratius John Ndejembi Mkoani Ruvuma inayotarajiwa kuanza kesho, Novemba 10, 2026, katika Wilaya ya Mbinga mkoani Ruvuma.
Amesema Wizara ya Viwanda na Biashara inashiriki moja kwa moja katika usimamizi wa mfumo huo kupitia Bodi ya Usimamizi wa Stakabadhi za Ghala (WRRB), kwa kushirikiana na Wizara ya Kilimo, na AMCOS ili kuhakikisha mazao yanayohusika yanauzwa kwa kuzingatia taratibu zilizowekwa.
Akifafanua manufaa ya mfumo huo, Mhe. Kapinga amesema unasaidia kuongeza ushindani wa bei za mazao, akitolea mfano wa kunde na mbaazi ambazo, kwa mujibu wa maelezo yake, awali zilikuwa zikiuzwa kwa Sh. 200 hadi 300 lakini kupitia mfumo huo zimeweza kufikia bei ya Sh. 1,400 hadi 1,500.
Aidha, amesema mfumo huo unamwezesha mkulima kufahamu kiasi cha mazao alichouza na fedha anazotarajia kupata, hivyo kuongeza uwazi na kupunguza uwezekano wa udanganyifu katika biashara ya mazao.
Aisha Mhe Kapingaamesema kuwa Mfumo wa Stakabadhi za Ghala una mchango katika kuweka kumbukumbu sahihi za mazao yanayouzwa nje ya nchi na kuongeza thamani ya bidhaa za Tanzania, huku Wizara ikiendelea kushirikiana na wadau kuboresha mazingira ya biashara na kukuza shughuli za wafanyabiashara nchini.
Akizungumzia kuhusu ziara hiyo Mhe Kapinga amesema akiwa wilayani Mbinga Makamuwaa Rais atatembelea na kukagua mradi wa ujenzi wa maghala ya kuhifadhi chakula, Ujenzi wa hospitali ya halmashauri ya wilaya ya mbinga, kukagua Barabara ya Amani Makoro Ruanda, na kuzungumza na wananchi wa Mbinga.
ziara hiyo ya Makamu wa Rais inatarajia kuongeza fursa za Kibiashara hususani Kwa mikoa ya Nyanda za juu kusini ambapo Kwa sasa Serikali inatarajia Kijana reli ya kutoka Mtwara hadi Ruvuma Kwa ajili ya usafirishaji wa makaa ya mawe na Chuma Kutoka mchuchuma na Liganga sambamba na uboreshaji wa bandari ya Nyasa ili kuchechemua uchumi.
Mipango mingine ni pamoja na Ujenzi wa kiwanda kiwanda unga kwenye halmashauri ya wilaya ya Mbinga na Ujenzi wa Maeneo ya Viwanda Kigonsera.





Post A Comment: