Na Denis Chambi, Tanga.

Mstahiki Meya wa Jiji la Tanga, Mhe. Seleboss Mustafa, amempongeza Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Balozi Dkt Batilda Burian, kwa kutilia mkazo suala la usafi wa mji, ikiwa ni pamoja na kuanzisha kampeni ya usafi ya kila siku ya  jumamosi ya kwanza ya mwezi, inayoitwa "Dkt. Batilda Mazingira Day"

Mstahiki Seleboss ametoa pongezi hizo kwenye mkutano wa Baraza la Madiwani la kupokea  taarifa za kata, kwa robo ya kwanza ya mwaka wa fedha 2026/2027, wakati akitambua michango ya wadau wa usafi na utunzaji wa mazingira katika jiji la Tanga.

Meya Seleboss, ambaye pia ni Diwani wa kata ya Nguvumali, amesema Halmashauri itaienzi siku hiyo, na kuwataka Watendaji wa Halmashauri kuhakikisha wanajipanga ili siku hiyo isimamiwe vizuri, huku akiwataka na Waheshimiwa madiwani kuwa na siku za jumamosi za usafi katika kata zao.

Mhe. Seleboss ametumia mkutano huo kutoa vyeti vya pongezi kwa Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Mhe. Balozi Dkt Batilda Burian, Mkuu wa Wilaya ya Tanga, Mhe. Edwin Mathew, baadhi ya Watendaji na wadau wengine, huku akiahidi kwa wakati mwingine, kuboresha utoaji huo wa vyeti ili uendane na utoaji wa kiwango cha pesa taslimu kwa wanaofanya vizuri.

Katika mkutano huo, Mstahiki Meya alimtambulisha rasmi Mkurugenzi wa Jiji la Tanga Bw. Philemon Mwita Magesa, ambaye huu ni mkutano wake wa kwanza tangu ahamie katika Jiji la Tanga, akitokea Halmashauri ya Wilaya ya Namtumbo, mkoani Ruvuma.

Moja ya wadau waliopata cheti na kupongezwa kwenye mkutano huo, ni Mwakilishi wa kampuni ya ujenzi ya Hassan Construction, inayofanya kazi kata ya Ngamiani kaskazini, ambayo imejitolea mifuniko 160 ya mfereji, na kuahidi kujengea mfereji wenye urefu wa mita 120. Kampuni hiyo pia imekuwa ikishiriki usafi wa msaragambo kwa kuwatoa wafanyakazi wake zaidi ya hamsini kujiunga na jamii kwenye zoezi hilo.




Share To:
Next
This is the most recent post.
Previous
Older Post

Post A Comment: