Na Denis Chambi Tanga,

WANANCHI wameshauriwa kuwa na desturi ya kunywa maziwa mara kwa mara ili kuweza kuimarisha afya zao kutokana na Madini, vitamini na virutubisho mbalimbali vinavyopatikana ndani yake hali ambayo itasaidia pia kuimarisha afya ya akili.

Wito huo umetolewa na Meneja masoko kutoka Bodi ya maziwa Tanzania Joseph Semu wakati akieleza hali ya uzalishaji wa maziwa kwa sasa mbele ya Naibu katibu mkuu Wizara  ya Kilimo Profesa Petter Msoffe wakati alipotembelea Banda lao katika maadhimisho ya chakula Duniani yanayofanyika kitaifa mkoani Tanga ambapo amesema kuwa  hali ya unywaji wa maziwa kwa wananchi ipo chini ukilinganisha na kiwango kinachotakiwa kwa mwaka

"Hali ya uzalishaji wa maziwa kwa sasa ni Lita Bilion 4.2 wakati mahitaji ni Lita Bilion 13 tuko chini na hatua zinaendelea kufanyika ikiwemo Serikali kupitia mradi mkubwa  wa mageuzi ya tathnia ya maziwa nchini ambao utakuja kuongeza uzalishaji wa kuboresha mifumo ya ukusanyaji na uchakataji wa maziwa nchini kwa kuboresha vituo ambavyo vinatumika kuimarisha mifugo  ili waweze kupatikana N'gombe bora lengo pia ni kumpunguzia mfugaji gharama za ufugaji anazotumia " amesema.

Semu amesema kuwa kwa wastani mtu kwa mwaka anatakiwa kutumia Lita 200 lakini kiwango hicho kipo chini ambapo kwa sasa zinatumika Lita 75 pekee hali ambayo wananchi wanapaswa kuhamasika zaidi.

Afisa Masoko kutoka Bodi ya Maziwa Tanzania Joseph Semu akitoa elimu ya unywaji wa maziwa kwa watoto wakati walipotembelea Banda lao kwenye maadhimisho ya siku ya chakula Duniani yanayoendelea kufanyika Mkoani Tanga 

"Tunahamasisha wananchi kuendeleza utamaduni wa kupenda kunywa maziwa zipo faida nyingi ambazo zinaambatana na unywaji wa maziwa, ndani ya maziwa kuna Madini, protini na Kila aina ya virutubisho vinavyosaidia mwili wa binadamu na kustawisha afya ya akili ndio maana tunahamasisha katika familia angalau kwa mtoto Kila anapopata chakula asikose glasi ya maziwa" amesema Semu.

Meneja huyo ameeleza kuwa Hadi kufika hasa Tanzania ina jumla ya vituo 275 vya kukusanya maziwa  usindikaji wa maziwa ukiongezeka kwa mwaka hadi Lita Milioni 101.5 wakati uwekezaji tukiendelea kukua na kufikisha viwanda 187 uzalishaji ukiongezeka na kufikia Bilion 4.2.
Naibu katibu mkuu Wizara ya Kilimo Profesa Petter Msoffe (kushoto) akizungumza na Meneja masoko kutoka Bodi ya maziwa Tanzania Joseph Semu wakati alipotembelea Banda lao kwenye maadhimisho ya siku ya chakula Duniani yanayofanyika Kitaifa mkoani Tanga.

"Mpaka sasa vituo vya kukusanya maziwa vimefikia 275 nchini kote ambako Hawa wachakataji wanakwenda kuchukua na kupeleka kwenye viwanda  lakini pia usindikaji wa maziwa umeongezeka  mpaka sasa tunasindika wastani wa Lita Milion 101 lakini hata viwanda vyenyewe vimeendelea kuongezeka nchini vikubwa na vidogo Hadi kufikia 187"

Kwa upande wake Afisa mauzo na  masoko kutoka Kiwanda cha Maziwa cha Tanga Fresh  Nassoro Mkutu amesema kuwa wanaendelea kuboresha bidhaa hiyo ambayo  imekuwa ikitumika ndani na nje ya nchi ili kuwavutia zaidi wateja.

Afisa Masoko kutoka Kiwanda cha Maziwa cha Tanga Fresh Nassoro Mkutu (kulia) akitoa maelezo kwa Naibu katibu mkuu Wizara ya Kilimo Profesa Petter Msoffe wakati alipotembelea Banda lao kwenye maadhimisho ya siku chakula Duniani yanayofanyika kitaifa mkoani Tanga 

"Tunaendelea kupambana kama Tanga Fresh kuhakikisha ubora wa maziwa yetu unabaki kama ilivyokuwa siku zote ili bidhaa zetu ziendelee kupendwa ndani na nje ya nchi" amesema Afisa huyo.
Share To:
Next
This is the most recent post.
Previous
Older Post

Post A Comment: