
Na; Mwandishi Wetu- Morogoro
Ujumbe kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Uratibu na wenye ulemavu ukiongozwa na Dkt. Salim Manyata Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Usimamizi wa Maafa pamoja na kamati ya Maafa ya Mkoa wa Morogoro, imetembelea maeneo korofi na yenye kuathirika zaidi na madhara yatokanayo na mvua katika ziara maalum ya kikazi ya kufanya ukaguzi na ufuatiliaji wa utekelezaji wa maelekezo yaliyotolewa kwa Mikoa kuhusu kujiandaa na kukabiliana na madhara ya El Nino tarehe 29 Septemba 2026.
Maeneo yaliyotembelewa ni Pamoja na eneo la mto Ngerengere katika eneo la Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo (SUA) ambapo kamati imejionea kazi maalum inayoendelea ya kusafisha mto kwa ajili ya kuongeza kina na upana wa mto huo kunusuru athari zinazoweza kujitokeza kutokanana na Mvua za Elnino zinazotabiriwa kunyesha.
Vilevile, kamati ilitembelea eneo lililopo kata ya Kihonda mtaa wa Azimio ambapo maji ya naingia kwenye makazi ya watu katika misimu tofauti ya Mvua kutokana na maji kukosa njia sahihi za kupita.
Aidha, zoezi la kufukua mifereji linaendelea kufanyika na taasisi husika chini ya usimamizi na uratibu wa Mkoa.
</








Post A Comment: