Kulea mtoto kwa maadili mema na kumpa kila hitaji la msingi ni ndoto na furaha ya kila mzazi, lakini pale mwanao anapogeuka kuwa janga la familia, ukaidi unapotawala, na anapojiunga na magenge ya uhalifu na matumizi ya dawa za kulevya, maisha ya wazazi hugeuka kuwa msiba wa kila siku.

Kwa zaidi ya miaka mitatu, mwanangu wa kiume aliyekuwa mwenye nidhamu na aliyefanya vizuri shuleni alibadilika ghafla. Alianza kutoroka shule, kuvuta bangi, na hatimaye kujiunga na kundi la vijana wa mtaani waliokuwa wakifanya wizi na kuwapiga watu nondo usiku.

​Kila nilipojaribu kuongea naye kwa wema, alinijibu kwa matusi, vitisho, na hata kutaka kunipiga. Nilitumia fedha nyingi kumpeleka kwenye vituo vya kuacha dawa za kulevya (rehab) na kumlipia dhamana mara kadhaa polisi pale alipokamatwa na uhalifu, lakini kila alipotoka alirudia tabia zile zile kwa kasi kubwa zaidi.

Nyumbani kwangu kuligeuka kuwa kero; alianza kuiba vyombo vya ndani, nguo, na vifaa vya elektroniki ili kwenda kuuza kwa bei ya kutupwa apate fedha za kununulia dawa za kulevya.

Nilibaki nikilia usiku na mchana, nikitarajia muda wowote kuletewa taarifa za kifo chake kutoka kwa wananchi wenye hasira kali au polisi, huku masimango ya majirani yakizidi kuwa makali. SOMA ZAIDI.
Share To:

Post A Comment: