Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT), Bw. Emmanuel Tutuba (kulia) akimueleza jambo Afisa Kurugenzi ya Usimamizi wa sarafu BoT, Bw. Shadrack Mapunda, wakati alipotembelea banda la Benki Kuu ya Tanzania (BoT) katika Maonesho ya 50 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam (Sabasaba), yenye Kaulimbiu ya "Maonesho ya Biashara ya Kimataifa Sabasaba ni Fahari ya Tanzania", yanayofanyika katika viwanja vya Mwl. J.K Nyerere, jijini Dar es Salaam.
Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT), Bw. Emmanuel Tutuba akioneshwa jambo na Meneja wa Idara ya Mawasiliana BoT, Bi. Victoria Msina wakati alipotembelea banda la Benki Kuu ya Tanzania (BoT) katika Maonesho ya 50 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam (Sabasaba), yenye Kaulimbiu ya "Maonesho ya Biashara ya Kimataifa Sabasaba ni Fahari ya Tanzania", yanayofanyika katika viwanja vya Mwl. J.K Nyerere, jijini Dar es Salaam.
Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT), Bw. Emmanuel Tutuba (kulia) akimsikiliza Afisa wa Benki Kuu Bw. Vitus Chaila, wakati alipotembelea banda la Benki Kuu ya Tanzania (BoT) katika Maonesho ya 50 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam (Sabasaba), yenye Kaulimbiu ya "Maonesho ya Biashara ya Kimataifa Sabasaba ni Fahari ya Tanzania", yanayofanyika katika viwanja vya Mwl. J.K Nyerere, jijini Dar es Salaam.
Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT), Bw. Emmanuel Tutuba (kulia) akimueleza jambo Afisa mitihani wa Chuo cha Benki Kuu, Bi. Beatha Rwimo, wakati alipotembelea banda la Benki Kuu ya Tanzania (BoT) katika Maonesho ya 50 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam (Sabasaba), yanayoendelea katika Viwanja vya Mwl. J.K Nyerere, jijini Dar es Salaam.
Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT), Bw. Emmanuel Tutuba (kulia) akimueleza jambo Afisa mitihani wa Chuo cha Benki Kuu, Bi. Beatha Rwimo, wakati alipotembelea banda la Benki Kuu ya Tanzania (BoT) katika Maonesho ya 50 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam (Sabasaba), yanayoendelea katika Viwanja vya Mwl. J.K Nyerere, jijini Dar es Salaam.
Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT), Bw. Emmanuel Tutuba (kulia) akiwaeleza jambo Afisa Utumishi BoT, Bi. Nancy Chengula na Msimamizi wa Mfuko wa ufadhili wa masomo wa mwalimu nyerere, Bi. Imelda Mzokolo wakati alipotembelea banda la Benki Kuu ya Tanzania (BoT) katika Maonesho ya 50 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam (Sabasaba), yenye Kaulimbiu ya "Maonesho ya Biashara ya Kimataifa Sabasaba ni Fahari ya Tanzania", yanayofanyika katika viwanja vya Mwl. J.K Nyerere, jijini Dar es Salaam.
Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT), Bw. Emmanuel Tutuba (kushoto) akiwaeleza jambo Meneja Masoko ya Fedha Bw. Lameck Kakulu, Afisa wa Benki BoT, Bw. Bikongo Mussa, Mchambuzi wa masuala ya fedha- Bw. Enthusiasm Mwagala wakati alipotembelea banda la Benki Kuu ya Tanzania (BoT) katika Maonesho ya 50 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam (Sabasaba), yenye Kaulimbiu ya "Maonesho ya Biashara ya Kimataifa Sabasaba ni Fahari ya Tanzania", yanayofanyika katika viwanja vya Mwl. J.K Nyerere, jijini Dar es Salaam.
Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT), Bw. Emmanuel Tutuba (kushoto) akimsikiliza
Mtaalamu wa Mifumo BoT, Bw. Dotto Namkaa wakati alipotembelea banda la Benki Kuu ya Tanzania (BoT) katika Maonesho ya 50 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam (Sabasaba), yenye Kaulimbiu ya "Maonesho ya Biashara ya Kimataifa Sabasaba ni Fahari ya Tanzania", yanayofanyika katika viwanja vya Mwl. J.K Nyerere, jijini Dar es Salaam. Wengine ni maafisa wa Benki Kuu Bw. Fredriki Mwakuu na Bi. Doreen Kabuche.


****************

NA EMMANUEL MBATILO, DAR ES SALAAM

Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania (BOT) amepongeza mafanikio yanayoendelea kupatikana katika Maonesho ya 50 ya Kimataifa ya Biashara ya Dar es Salaam (Sabasaba), akisema yameendelea kuwa jukwaa muhimu la kukuza biashara, uwekezaji na uchumi wa Taifa.

Akizungumza leo Julai 10 baada ya kutembelea mabanda mbalimbali ya maonesho hayo, Gavana amesema Sabasaba imeendelea kutoa fursa kwa Watanzania kujifunza, kupata huduma mbalimbali na kujionea bidhaa pamoja na teknolojia mpya zinazochochea maendeleo ya kiuchumi.

Amesema maonesho ya mwaka huu, yanayoadhimisha miaka 50 tangu kuanzishwa kwake, yamevutia ushiriki wa mataifa zaidi ya 25, hali inayoonesha hadhi yake ya kimataifa na mchango wake katika kukuza biashara za ndani na nje ya nchi.

Akizungumzia sera ya fedha, Gavana amesema uamuzi wa Benki Kuu kuweka kiwango cha riba cha asilimia 6.25 umefanyika kwa kuzingatia hali ya uchumi na lengo la kuhakikisha utulivu wa bei pamoja na kuimarisha shughuli za uzalishaji.

Ameeleza kuwa hatua hiyo inalenga kuhakikisha ukwasi wa kutosha katika mabenki ya biashara ili yaendelee kutoa mikopo kwa sekta binafsi na wakati huo huo kudhibiti mfumuko wa bei ubaki ndani ya lengo la asilimia 3 hadi 5.

Aidha, amesema kuanza kwa msimu wa mavuno kunatarajiwa kuimarisha thamani ya shilingi ya Tanzania, hali itakayowawezesha wakulima kupata bei nzuri ya mazao yao na kuongeza manufaa kwa wafanyabiashara wanaouza bidhaa katika masoko ya nje.

Katika hatua nyingine, Gavana amesema Benki Kuu ipo katika hatua za mwisho za kuandaa mfumo wa kisheria utakaosimamia matumizi ya sarafu za kidijitali na mali za mtandao (virtual assets), ikiwemo Bitcoin na stablecoins.

Amesema tayari Benki Kuu imeandaa waraka wa awali (concept note), pamoja na rasimu ya sheria na kanuni, ambazo zinaendelea kuwasilishwa katika taasisi husika, ikiwemo Wizara ya Fedha, Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Baraza la Mawaziri na baadaye Bunge kwa hatua za mwisho za kupitishwa.

Gavana amesema uwepo wa sheria hizo ni muhimu ili kukabiliana na vihatarishi vinavyoweza kujitokeza kupitia matumizi ya sarafu za kidijitali, ikiwemo utakatishaji wa fedha haramu, ufadhili wa ugaidi na kulinda uwekezaji pamoja na mitaji ya Watanzania.

Kwa upande wa elimu ya fedha, Gavana amesema ameridhishwa na mwitikio mkubwa wa wananchi wanaotembelea mabanda ya Benki Kuu na Chuo cha Benki Kuu kupata elimu kuhusu huduma za kifedha na usimamizi wa fedha binafsi.

Amesema BOT imeandaa programu maalumu ya elimu ya fedha itakayofanyika mwezi Novemba mwaka huu, ambapo tayari zaidi ya washiriki 200 wamejiandikisha kushiriki mafunzo hayo.

Share To:

OSCAR ASSENGA

Post A Comment: