NAIBU Waziri wa Madini na Mbunge wa Jimbo la Longido Mkoani Arusha,Dkt Steven Kiruswa  amesema katika kipindi cha miaka mitano ijayo cha uongozi wake anawiwa na kuhakikisha anatekeleza vipaumbele 16 katika kukamilisha miradi ya maendeleo katika Jimbo hilo.

Dkt Kiruswa alisema hayo katika mkutano wa hadhara wenye lengo la kuwashukuru wananchi wa Jimbo la Longido kwa kukichagua chama chake cha Chama Cha Mapinduzi{CCM},Mgombea Urasi wa chama hicho Rais Samia Suluhu Hassan na Makamu wake Dkt Emmanuel Nchimbi,Mbunge na Madiwani wote wa chama hicho katika mkutano uliohudhuriwa na viongozi mbalimbali wa chama na serikali katika ngazi ya tawi,kata na wilaya uliofanyika katika uwanja wa Longido Polisi.

Alisema moja ya vipaumbe ambavyo anataka kuvifanyia kazi katika kipindi miaka mitano ya ubunge wake ni pamoja na kukamilisha ujenzi wa shule za msingi na sekondari katika kata zote za Jimbo hilo,kubuni miradi ya ajira kwa vijana,kukamilisha mradi wa maji wa chanzo cha Loormokerian Kijiji cha Oltepesi,kuchimba visima vya maji Kiseriani na Orkesumet.

Waziri Kiruswa alitaja kipaumbe kingine ni pamoja na ukarabati na ufunguaji wa barabara zilizo chini ya Wakala wa Barabara Mjini na Vijijni{TARURA} kwenye maeneo ynye vipaumbele,uendelezaji wa shule shikizi katika kata ambazo hazina ikiwa ni njia ya kupunguza umbali mrefu kwa watoto kwenda na kurudi shule na kujikinga na wanyama wakali.

Alisema ana uhakika ndani ya muda huo vipaumbele alivyovioanisha vitakuwa vimekamilika kwa kushirikiana na wananchini,serikali kuu,wadau wa maendeleo na wafadhili wa ndani na nje lengo kuu ni kutaka kuwapelekea huduma wananchi.

Aidha alitumia nafasi hiyo kuwashukuru wananchi kwa kumpa kura nyingi Rais Samia Suluhu Hassan na kuwa Rais awamu ya sita na kusema kuwa uamuzi walioufanya umeiheshimisha Longido kwani imekuwa wilaya ya kwanza kwa kutoa kura Nyingi Mkoani Arusha.

Waziri Kiruswa alisema kutokana na hali hiyo aliwaomba wananchi wa Longido kuwa wamoja na watulivu katika kuiletea maendeleo Longido na kumwombea afya njema Rais ili aweze kuendelea kuiongoza nchi kwa amani na upendo.

''Nawaomba wananchi wa Longido tuiombe nchi amani na tumwombee Rais wetu Samia Suluhu Hassan afya njema kwani amekuwa mstari wa mbele kuiendeleza Longido hivyo kila mmoja kwa imani yake ya kiislamu na kikrusto anapaswa kufanya hivyo''alisema Kiruswa

Naye Mkuu wa wilaya ya Longido,Salumu Kally amesema ni wakati wa wana Longido kushirikiana na Mbunge katika kuiletea maendeleo Jimbo hilo na kusema kuwa mifarakano mara nyingi hurudisha nyumba maendeleo hivyo hataki kuliona hilo likitokea.

Naye Mbunge wa Monduli,Joseph Isack na Mbunge wa Ngorongoro Yannick Ndoinyo wote waliwaomba wananchi wa Longido kushirikiana na Mbunge wao Kiruswa kwani mbunge huyo ni mpenda watu na mpenda maendeleo hivyo wasidhubutu kuipoteza lulu hiyo kwa namna yoyote ile kwani watakuwa wamefanya maksa makubwa sana,

 

Share To:
Next
This is the most recent post.
Previous
Older Post

Post A Comment: