Watanzania wamehamasishwa kuendelea kumuombea Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe Dkt. Samia Suluhu Hassan ili aweze kupata utulivu wa kuliongoza Taifa la Tanzania kwa amani, upendo na mshikamano.

Rai hiyo imetolewa leo Aprili 19, 2026 na Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya MASHILI COMPANY LIMITED ambaye pia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Mradi wa Uchenjuaji Dhahabu wa (Matinje Mining, Msilale Mining na Igurubi Mining) Ndg Peter Andrea Mashili aliposhiriki tamasha la Inland Festival lililoandaliwa na kanisa la Africa Inland Church Tanzania - AIC Wilayani Nzega katika mkoani Tabora.

Mashili amesema kuwa Mhe Rais Dkt. Samia anafanya kazi kubwa ya kuifungua nchi na kuleta maendeleo hivyo ni jukumu la wananchi kuhakikisha wanamuombea ili aweze kuongoza kwa busara na mshikamano wa kitaifa.

Pia Mashili amewataka viongozi wa dini na wananchi wote wa wilaya ya Nzega kumuombea Mbunge wa jimbo la Nzega Mjini Mhe Hussein Bashe ili aweze kuitumikia nafasi yake kwa uaminifu na weledi katika bunge la Tanzania.

Amesisitiza umuhimu wa kuwaombea viongozi wote katika nchi itasaidia kutangaza na kuhubiri amani jambo ambalo litalifanya Taifa la Tanzania kuwa na utulivu.

"Maombi ni silaha hivyo naendelea kusisitiza kuwaombea viongozi wetu kwani jambo hilo litarahisisha uenezaji wa injili na kuwafanya watanzania kuendelea kuwa na mshikamano wa kudumu" Amekaririwa Mshili

Katika tamasha hilo Peter Mashili amechangia jumla ya shilingi 3,200,000 kwa ajili ya kuunga mkono maboresho ya studio ya Inland Tv na ununuzi wa vifaa vya kurushia matangazo ya televisheni na redio ya kanisa hilo.

Share To:

OSCAR ASSENGA

Post A Comment: