Wananchi wametakiwa kupanda miti na kutunza Misitu nchini kwa maslahi mapana ya Taifa na mtu mmoja mmoja.

Wito huo umetolewa na Mkuu wa Mkoa wa Njombe Mhe. Antony Mtaka, Mkoani Njombe, kwenye zoezi la upandaji wa miti katika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa kama sehemu ya maadhimisho ya Mei Mosi 2026

Mhe. Mtaka amesema kuwa, Misitu ni nguzo muhimu kwa uchumi wa nchi hivyo nivyema ikalindwa kwa wivu mkubwa na kutoichoma moto.

 Amesisitiza kuwa zoezi la upandaji miti liendane sambamba na upandaji wa miti ya matunda hususani Miparachichi ambayo inasoko kubwa ndani na nje ya nchi. 

Zoezi hilo la upandaji miti linalojulikana kwa Jina la "27 ya KIJANI, MTI WA MAMA" pamoja na viongozi wengine limeudhuriwa na rais wa Shirikisho la vyama vya Wafanyakazi (TUCTA) Cde. Tumaini Nyamhokya, Mkurugenzi Msaidizi Utawala Bi. Violeth Mlinga kutoka Wizara ya Maliasili na Utalii na watumimishi mbalimbali wa serikali.


Share To:

OSCAR ASSENGA

Post A Comment: