Na OWM - TAMISEMI, Dar es Salaam

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OWM-TAMISEMI) Mhe. Prof. Riziki Shemdoe, amemshukuru  Waziri Mkuu Mhe. Dkt. Mwigulu Nchemba kwa kuadhimisha miaka 62 ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kukagua ujenzi wa miradi ya maendeleo ya daraja jipya la Mkwajuni, daraja jipya la Kigogo ikiwa ni pamoja na kutatua kero za wananchi wa jiji la Dar es Salaam.

Prof. Shemdoe ametoa shukurani hizo leo Aprili 26, 2026 jijini Dar es Salaam       wakati akizungumza na wananchi wa jiji la Dar es Salaam katika Uwanja wa Shule ya Msingi Msimbazi mara baada ya Mhe. Waziri Mkuu kukagua miradi hiyo ya maendeleo, ikiwa ni sehemu ya Maadhimisho ya Miaka 62 ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

“Mhe. Waziri Mkuu nakushukuru sana kwa uamuzi wako wa kuadhimisha miaka 62 ya Muungano kwa kukagua miradi ya maendeleo na kutatua kero za wananchi wa Dar es Salaam tena siku ya Jumapili,” Prof. Shemdoe amesisitiza.

Prof. Shemdoe amefafanua kuwa, uwanja umefurika idadi kubwa ya wananchi licha kuwa ni siku ya jumapili kwasababu wana Imani na wanafahamu kuwa Mhe. Waziri Mkuu utawasikiliza kero zao na kuzitatua hivyo watarejea kwenye makazi yao na tabasamu la kudumu.

Akizungumzia mwendelezo wa Serikali kutatua kero za wananchi, Prof. Shemdoe amesema siku chache zilizopita Mhe. Waziri Mkuu alimtuma kuja jijini Dar es Salaam kushuhudia utiaji wa saini wa Mradi wa Uendelezaji wa Bonde la Mto Msimbazi utakaogharimu zaidi ya  Shilingi Bilioni 190, fedha ambazo ziliidhinishwa na Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan na kuongeza kuwa   mradi huo ni sehemu muhimu kwa uchumi na mazingira mkoani Dar es Salaam.

“Nichukue fursa hii kumshukuru Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuridhia kuletwa kwa fedha za kutekeleza Mradi wa Uendelezaji wa Bonde la Mto Msimbazi, lakini pia nikushukuru wewe Mhe. Waziri Mkuu kwani nikiwa Katibu Mkuu TAMISEMI nakumbuka ulikuwa ukiongoza vikao vya Serikali na wadau wa Maendeleo vilivyowezesha kupatikana kwa fedha hizo ,” amesema Prof. Shemdoe.

Share To:

Post A Comment: