Waziri Wa Nchi, Ofisi ya Rais, Mipango na Uwekezaji, Prof. Kitila Mkumbo akiwasilisha Hotuba ya Bajeti kwa Mwaka wa Fedha 2026/2027.

....

Ofisi ya Rais, Mipango na Uwekezaji na taasisi zilizo chini yake imeliomba Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuidhinisha jumla ya shilingi trilioni 1.79 na matumizi ya jumla ya shilingi bilioni 144.8 kwa ajili ya ofisi hiyo kwa mwaka wa fedha 2026/2027.

Hayo yameelezwa leo Aprili 16, 2026 na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Mipango na Uwekezaji, Profesa Kitila Mkumbo wakati akiwasilisha hotuba ya bajeti ya wizara yake bungeni jijini Dodoma.

Profesa Mkumbo amesema kati ya fedha hizo, shilingi bilioni 126 ni kwa ajili ya matumizi ya kawaida na shilingi bilioni 18.8 kwa ajili ya miradi ya maendeleo.

Share To:

Alex Sonna

Post A Comment: