Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge Tawala wa Mikoa na Serikali wa Mitaa - TAMISEMI, wameridhishwa na kupongeza utekelezaji wa mradi wa ujenzi wa shule mpya ya sekondari ya wasichana Longido Samia Girl's, wilaya ya Longido Mkoa wa Arusha, mradi uliotekelezwa na Serikali kwa gharama ya shilingu Bilioni 4.4, kupitia programu ya SEQUIP.
Akizungumza mara baada ya kukagua mradi huo mapema leo machi 17,2026, Mwenyekiti wa Kamati hiyo Mhe. Florent Kyombo (Mb), licha ya kuridhishwa na ubora wa mradi huo, ameipongeza Serikali ya awamu ya sita chini ya Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kutoa fedha nyingi za kuboresha miundonu ya elimu nchini huku Mkoa wa Arusha ukiwa ni miongoni mwa wanufaika.
Ameweka wazi kuwa, lengo la serikali ni kuhakisha watoto wa kitanzania wanapata elimu kwenye mazingira rafiki na dhamira ya dhati Dkt.Samia ni kuwahamasisha watoto wa kike nchini kusoma masomo ya Sayansi ili kuzalisha watalamu wengi katika fani za Sayansi.
Hata hivyo wajumbe hao, wameshauri mkoa kuwa na msimamizi wa majengo 'Estate Manager' atakayekuwa na dhamani ya kusimami majengo yote ya serikali yaliyokamilika, ili kuhakikisha yanaendelea kutunzwa na kuendelea kuwa bora pamija na kushugulikia masuala ya ukarabati wa majengo hayo.
Naye mkuu wa wilaya ya Longido Mhe. Ally Kali, amewashukuru wajumbe wa kamati hiyo kwa niaba ya wananchi wake, kwa kuwatembelea na kukagua mradi huo wa shule, mradi ambao amekiri ni muhimu kwa watoto wa jamii ya Kimaasai, jamii ambao hapo awali wasichana wengi walikosa nafasi ya kupata elimu.
Mhe. Kali, amesisitiza kufanyia kazi maelekezo na ushauri ulmntolewa na wajumbe ikiwa ni pamoja na kupeleka maombi ya mahitaji ya shule hiyo kwenye Kamati ya Bajetii ili yaingizwe kwenye bajeti ya mwaka ujao wa fedha
Awali shule ya wasichana Longdo Samia Girl ni miongoni mwa shule 26 za kimkoa,ukiwa na lengo la kuongeza idadi ya shule na kuboresha mazingira ya ujifunzaji na ufundishaji nchini, iliyoanza kupokea wanafunzi mwaka 2024 ina wanafunzi 681 wa kidato cha 1-6 kwa mchepuo wa Sayansi.










Post A Comment: