WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa{TAMISEMI}Professa Riziki Shemdoe amesema kuwa fedha za mradi wa shilingi Bilioni 82.5 za ujenzi wa Miundombinu ya barabara inayozunguka uwanja wa AFCON ni fedha za mapato ya ndani hivyo wananchi wa Mkoa wa Arusha wametakiwa kuitunza miundombinu hiyo.
Professa Shemdoe alisema hayo jana Jijini Arusha wakati wa utiaji saini kati ya Wakala wa Barabara Mjini na Vijijini{TARURA} na Mkandarasi wa mradi huo kampuni ya CRJE ya Nchini China shughuli iliyofanyika eneo la karibu ya uwanja na kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali wa Chama Cha Mapinduzi{CCM}ngazi ya kata hadi Mkoa,viongozi wa serikali,viongozi wa dini na wananchi wa Mkoa wa Arusha.
Alisema mashindano ya AFCON ni mashindano muhimu sana Afrika na yanaangaliwa na mamia ya watu wengi Duniani na hivyo basi Miundombinu yeke ya kuzunguka uwanja huo yanapaswa kuwa yenye ubora mzuri wenye kuwafutia watu wote wataokwenda kuangalia mashindano hayo na ndio maana Rais Samia Suluhu Hassan ameridhia utolewaji wa fedha hizo kutoka mapato ya ndani.
Waziri alisema kutokana na umuhimu ulionyeshwa na Rais wa kutoa fedha hizo kwa ajili ya ujenzi wa Miundombinu inayozunguka uwanja huo,wananchi wote wa Mkoa wa Arusha wanapaswa kuwa walinzi wa Miundombinu hiyo kwa maslahi ya Umma na mradi huo unapaswa kukamilika mapema mwezi Mei mwakani na kusiwe na visingizio.
Alisema viongozi wa Chama,serikali na wananchi wa Mkoa wa Arusha wanapaswa kumshukuru Rais kwa kujitoa kwa ajili ya ujenzi wa uwanja huo ambao kwa sasa ujenzi wake umefikia asilimia 75 na pia kutoa fedha nyingine kwa ajili ya Mindombinu ya Barabara inayozunguka uwanja hyuo kwani uamuzi huo unapaswa kupongezwa na kila mmoja.
''Utekelezaji wa mradi huu ni jitihada za serikali chini ya Rais Samia Suluhu Hassan za kutaka mashindano ya AFCON kuchezwa katika mazingira mazuri na yenye mvuto sambamba na Miundombinu ya barabara kuwa katika hali ya ubora na kuvutia''alisema Shemdoe
''Wananchi wote wote Mkoani Arusha na Mikoa ya jirani wanatakiwa kuwa wasimamizi wa mradi huu na maradi unaposuasua wanapaswa kutoa taarifa sehemu husika ili hatua ziweze kuchukuliwa kwani mradi huu ni wetu sote''alisema
Naye Mtendaji Mkuu wa Tarura,Mhandisi Victor Seif alisema ujenzi wa Miundombinu ya Barabara za kuelekea na kuzunguka uwanja wa mpira utakaotumika katika mashindano ya Kombe la Mataifa ya Afrika AFCON 2027 katika Jiji la Arusha umegharimu kiasi hicho cha fedha na Barabara ya km 19.9 ambayo itakuwa na njia nne na mbili.
Mhandisi Seif alisema kuwa ujenzi wa uwanja umefikia zaidi ya asilimia 75 sambamba na ujenzi wa Miundombinu muhimu yenye umbali wa zaidi ya km 19.9 kwa kiwango cha lami kuelekea kwenye uwanja huo kutokea Barabara Kuu ya Arusha-Babati na Arusha Bypass na kuzunguka uwanja huo Mateves-Bondeni km 6.5,Km 1.5 njia nne na km 5 njia mbili kutoka barabara kuu Arusha -Babati,barabara ya Lendita km 2.75 njia nne ,barabara ya Essari km 2.45 2.45 njia nne zote kutoka barabara kuu ya Arusha Bypass na km 1.5 barabara kuzunguka uwanja.
Alisema baada ya mchakato wa ununuzi kukamilika,Kampuni ya M/s China Railway Construction Engineering Group kushinda zabuni na kupewa kazi hiyo ya ujenzi wa barabara kwa gharama ya zaidi ya shilingi Bilioni 82.5 kwa muda wa miezi 13 na kazi inapaswa kuanza aprill mosi mwaka huu na usimamizi wa ujenzi wa barabara hiyo utasimamiwa na kampuni ya M/s Afrisa Consulting ya Jijini Dar es Salaam kwa mkataba wenye thamani ya shilingi Bilioni 1.4
Naye Mbunge wa Jimbo la Arusha Mjini na Waziri wa Habari,Sanaa ,Michezo na Utamaduni,Poul Makonda alisema kuwa Jiji la Arusha lina kiu kubwa na barabara za lami kwani ni Jiji la mwisho kuwa na barabara za lami kwani Majiji yote Tanzania yana barabara za lami hivyo aliiomba Tarura kuhakikisha inafanya kila jitihada kutekeleza ahadi zake za ujenzi wa barabara za kiwango cha lami ili wananchi waweze kupitia kwa nyakati zote.
Makonda alisema na kumshukuru Rais kwa uamuzi wake wa kuridhia kutoa fedha shilingi Bilioni 82.5 kwa ajili ya Miundombinu ya kuzunguka uwanja wa AFCON na kusema kuwa uamuzi huo unapaswa kupongezwa na kuwataka wakazi wa Arusha kushukuru kwa hilo na kuwasihi wananchi watakaolipwa fidia kupokea fedha hizo bila kuleta manung'uniko.
Naye Mkuu wa Mkoa wa Arusha Amos Makalla ameahidi kuwasimamia wakandarasi wa ujenzi wa Miundombinu ya kuzunguka uwanja huo ili waweze kuimaliza kwa wakati na kuwataka wananchi kuwa mstari wa mbele kutoa taarifa pindi mkandarasi atakaonekana anafanaya kazi kwa kusuasua katika kutekeleza majukumu yake.














Post A Comment: