WATOA huduma za mionzi kwenye vituo mbalimbali vya afya nchini wameagizwa kuepuka kiwango kikubwa cha mionzi kwa wagonjwa na kwao ili kisiweze kuleta madhara zaidi

Hayo yalisemwa jana Jijini Arusha na Kaimu Mkuu wa Ofisi ya Kanda ya Tume ya Nguvu za Atomiki Tanzania (TAEC), Peter Pantaleo wakati wa kufunga mafunzo yaliyoshirikisha wataalam wa Radiolojia zaidi ya 90 yaliyotolewa na tume hiyo

Pantaleo alisema kiwango kikubwa cha mionzi kinamadhara zaidi kuliko kiwango kidogo hivyo wataalam hao wanapaswa kuepuka viwango hivyo vikubwa ili kuzuia madhara

Alisema pia watoa huduma hiyo lazima wajue pia kunawagonjwa wanaohitaji huduma hiyo kwa usalama zaidi ikiwemo kuwakinga wale walioambatana nao 

"Mafunzo haya ni muhimu kwa wataalam wa mionzi ili kuhakikisha usalama wao na kwa wale wanaopata huduma hiyo au kwa wale wanaokwenda hospitali"

Huku mkufunzi wa mafunzo hayo, Mungubariki Nyaki alisisitiza wataalam hao kuhakikisha wanatoa huduma nzuri kwa wagonjwa ikiwemo  kuzingatia matumizi sahihi ya mionzi hiyo

"TAEC itaendelea kutoa mafunzo katika kada mbalimbali katika kuhakikisha watoa huduma na wataalam wa mionzi wanajikinga na mionzi lakini pia huduma za mionzi ni salama hivyo wagonjwa wasiogope kwani mionzi imedhibitiwa"

Wakati huo huo baadhi ya washiriki wa mafunzo hayo Beatrice Mallya na Hussein Shabani walishukuru TAEC kwa kutoa mafunzo hayo ambayo yanakumbusha kutumia kwa usahihi mionzi hiyo pamoja na kuhakikisha vyumba vinavyotolea huduma hiyo vinakuwa vya kisasa zaidi

Huku  Shabani alisisitiza matumizi sahihi ya mionzi ndio chachu ya huduma bora kwa wagonjwa wanaofika hospalini kupata huduma hizo

Share To:

Post A Comment: