Na Munir Shemweta, WANMM MTWARA

 

Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Dkt Leonard Akwilapo leo tarehe 22 Desemba 2025 amekutana na kufanya mazungumzo na Mkuu wa mkoa wa Mtwara Kanali Patrick Sawala.

 

Mhe. Dkt Akwilapo ambaye yuko ziarani mkoani Mtwara amemueleza Kanali Sawala juhudi za wizara yake katika kushughulikia changamoto za sekta ya ardhi nchini.

 

"Sisi kama wizara tutazifanyia kazi changamoto zote za sekta ya ardhi na hapa Mtwara tayari tumeshaanza kuzifanyia kazi, lengo ni kutaka kuwaacha wananchi wetu wawe na furaha". Amesema

 

Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Kanali Sawala amempongeza Mhe. Dkt Akwilapo kwa kuaminiwa na Rais Mhe. Dkt Samia Suluhu Hassan kuteuliwa kuwa Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi wizara aliyoieleza kuwa ni nyeti kutokana na kugusa maisha ya kila mtu.

 

"Nikuahidi Mhe. Waziri sisi kama mkoa tutajitahidi kukusemea kwa yale yote mazuri unayofanya katika mkoa wetu". Amesema Kanali Sawala

Share To:
Next
This is the most recent post.
Previous
Older Post

Post A Comment: