Mgombea wa Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dkt. Samia Suluhu Hassan, ameahidi kuboresha utoaji wa elimu jumuishi ili kuwawezesha watoto wenye mahitaji maalum kupata elimu bora.

Akihutubia mkutano wa kampeni uliofanyika Septemba 24, 2025,  Ndanda, Wilayani Masasi, Dkt. Samia amesema anatambua changamoto zinazozikabili shule za wanafunzi wenye mahitaji maalum, ikiwemo Shule ya Luguleni, na ameahidi kuzitatua.

“Natambua hapa Ndanda, kule Luguleni kuna shule ya wenye mahitaji maalum ambayo nayo ina changamoto kadhaa. Shule haina uzio, haina gari la usafiri na pia inakabiliwa na upungufu wa vifaa vya kujifunzia kwa vitendo. Niwaahidi nitazitatua,” amesema Dkt. Samia.

Aidha, amesisitiza kuwa Serikali itaendelea na sera ya kutoa elimu bure kwa wote ili kuhakikisha kila mtoto nchini anapata nafasi ya kusoma bila vikwazo.

Share To:

Post A Comment: