KATIBU Mkuu Kiongozi  wa Baraza la Mapinduzi na Katibu Mkuu Kiongozi wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Mhandisi Zena Ahmed Said ameagiza  Jumuiya ya Wataalam wa Usimamizi wa Rasilimali Watu na Utawala katika Utumishi wa Umma (TAPA -HR) kuanzisha  mchakato wa uundwaji wa bodi ya taaluma kwa kada hiyo ili kuondoa sintofahamu  ya ukiukwaji wa maadili  na kuleta tija katika ufanisi wa kazi 

Agizo hilo lilitolewa leo Jijini Arusha na Mhandisi  Zena Ahmed Said wakati wa ufunguzi wa Mkutano Mkuu wa Kwanza wa Mwaka wa (TAPA-HR) wenye kauli mbiu ya mwelekeo mpya wa nafasi ya w ataalamu wa Usimamizi wa Rasilimali Watt na Utawala :Kusukuma  Mabadiliko, Kuendana na Mageuzi na Teknolojia kwaajili ya kuboresha huduma katika Utumishi wa Umma unaofanyika kwa siku nne.

Amesema  endapo bodi hiyo ikiundwa itaondoa malalamiko mengi ya ukiukwaji wa taaluma ikiwemo kukaa na Chuo cha Utumishi wa Umma ili kuwapa mahitaji ya kitaaluma ya  kada hiyo ili waweze kuhuisha na kuboresha maudhui na utaratibu wa kitaaluma wa kada ya maofisa rasilimali watu na maofisa utawala katika kuakisi mahitaji ya sasa kwamujibu wa miongozo iliyopo

Alisema pia Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora kufanyia kazi hoja iliyowasilishwa kuhusu kuhuisha muundo wa utumishi kwa maendeleo ya kada hiyo ili kuendana na kasi ya mabadiliko ya sasa ikiwemo kuendana na kasi na ari katika ufanisi wa kazi

"Muundo uliopo  ni wa zamani  unatakiwa uhuishwe ili ulete tija zaidi lakini pia bodi hii itawasaidia kupata uhalisia wa nidhamu pamoja na kuondoa malalamiko kwa baadhi ya maofisa wanaokiuka kanuni na miongozo ya utumishi wa umma"

Alisema pia wasimamie wajibu na haki za watumishi pamoja na rasilimali zilizopo mahali pa kazi ikiwemo kushauri waajiri kujiunga na kutumia kikamilifu mifumo ya kidigiti ambayo imesanifiwa na ofisi ya Rais , menejimenti ya utumishi wa umma na utawala bora ili kupunguza vitendo vya rushwa, kuimarisha uwajibikaji na ufanisi katika utoaji huduma kwa wananchi.

Aliongeza kuwa watumishi waandaliwe ili kuendana na kasi ya mabadiliko mbalimbali yanayoendelea kutokea katika taaluma zao ikiwemo mpango wa  mafunzo unaoendana na mpango wa taasisi za serikali katika utelezaji wa dira ya Taifa kwa mwaka 2025-2050 ikiwemo mpango wa kuridhishana madaraka ili kuondoa sintofahamu pale viongozi  wanapotaka kuteua watumishi wengine

Naye Kaimu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais, Menejimenti ya  Utumishi na Utawala Bora, Xavier Mrope  alisisitiza dira ya Taifa ya Maendeleo ya mwaka2025/ 2050 iliyozunduliwa na Rais itasaidia wataalam hao kuleta tija zaidi na kusisitiza kubadilika kutokana mabadiliko ya teknolojia inayokua kwa kasi  zaidi. 

Nate Mwenyekiti wa TAPA-HR,Grace Fransic amesema chama hicho kinalengo la ukuzaji wa taaluma zao lakini pia wanakabiliwa na changamoto waliyonayo ni changamoto ya muundo uliopitwa na wakati na kuiomba serikali kuboresha au kuhuisha muundo huo ili kuendana na mabadiliko ya sasa 

Huku Katibu  Tawala Msaidizi Menejimenti ya Ufuatiliaji na Ukaguzi Serikali za Mitaa Mkoa wa Arusha,Ramadhani Madeleka kwaniaba ya Katibu Tawala Mkoa huo, Missaile  Mussa alishukuru mkutano huo kufanyika Jijini Arusha na Kong kuwa usalama katika mkoa huo umeimarika

Mkutano huo umejumuisha washiriki zaidi ya 999 kutoka kada mbalimbali za maofisa rasilimali watu lakini pia walizindua tovuti ya Jumuiya hiyo pamoja na kutoa tuzo kwa wafanyakazi bora.










Share To:

Post A Comment: