Afisa Uhusiano ,Huduma kwa Wateja wa Shirika la Umeme (TANESCO) mkoa wa Kilimanjaro Bi Mwanaisha Mbita akikabidhji jiko la umeme kwa familia ya Mwalimu Mstaafu Rajabu Samweta ikiwa  ni sehemu ya uhamasishaji juu ya matumizi ya nishati nafuu kwa wananchi.
Bi Debora Mwamponda (Mwanamke Shupavu) akitoa elimu juu ya matumizi ya nishati nafuu ya kupikia kwa kutumia umeme kwa mmoja wa nananchi wakijiji cha Maendeleo kilichopo Chekereni katika wilaya ya Moshi 
Baadhi ya Wateja wa huduma ya umeme katika kijiji cha Muungano Chekereni kilichopo wilaya ya Moshi wakisiliza maelekezo kutoka kwa maafisa wa TANESCO mkoa wa Kilimanjaro ,Afisa Uhusiano ,Huduma kwa wateja Mwanaisha Mbita pamoja na Obadiah.
Baadhi ya Wananchi katika kijiji cha Muungano ,Chekereni wilaya ya Moshi wakifuatilia maelezo ikiwa ni pamoja na kuwasilisaha changamoto zao kwa maafisa wa Tanesco mkoa wa Kilimanjaro .
Afisa Uhusiano ,Hudumakwa wateja wa TANESCO mkoa wa Kilimanjaro akizungumza na wananchi katika eneo la Chekereni ,lililopo wilaya ya Moshi mkoa wa Kilimanjaro .

Na Dixon Busagaga Moshi

Katika hali isiyo ya kawaida lakini yenye mafunzo kwa jamii, mkazi wa Kijiji cha Maendeleo wilayani Moshi, Yusufu Samweta, ameeleza namna zawadi ya jiko la umeme kutoka Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) ilivyobadili maisha ya familia yake — si tu kwa kupunguza gharama za upishi, bali pia kwa kumaliza migogoro ya kifamilia iliyokuwa imeshamiri nyumbani kwake.

“Tulikuwa tunagombana na mke wangu kwa sababu chakula kilichelewa — moshi mwingi, kuni hazipatikani kwa wakati, watoto wanalia. Lakini tangu TANESCO waletee hili jiko, maisha yamebadilika. Tunakula kwa wakati, hakuna kelele, hakuna ugomvi… hata afya imeimarika,” alisema Samweta kwa hisia.

Kauli hiyo imekuja kufuatia kampeni ya TANESCO ya kusambaza elimu na vifaa vya matumizi ya nishati safi kwa wananchi, kupitia ushiriki wake kwa wanawake shupavu ikiwa ni sehemu ya kukutana na wanawake hao Agosti itatu mwaka huu katikamkoa wa Kilimanjaro.

Akizungumza kuhusu mpango huo, Afisa Uhusiano Huduma kwa Wateja wa TANESCO Mkoa wa Kilimanjaro, Bi. Mwanaisha Mbita, alisema kuwa lengo ni kutumia fursa ya tkuwawezesha wananchi kupata elimu ya matumizi ya nishati salama na kuhamasisha mabadiliko ya kijamii kupitia teknolojia rafiki kwa mazingira.

“Tunataka kuona wanawake na familia kwa ujumla wakijifunza kutoka kwa akina kina Samweta — kwamba jiko la umeme linaweza kuokoa muda, kuboresha afya, kuondoa migogoro ya kifamilia na pia kusaidia kutunza mazingira. Tunaamini nishati safi ni msingi wa maendeleo endelevu,” alisema Bi. Mbita.

Bi. Mbita aliongeza kuwa TANESCO inaendelea kutoa majiko ya mfano kwa baadhi ya familia ambazo bado hazijaanza kutumia umeme kwa ajili ya mapishi, huku ikiwapa mafunzo ili wawe mabalozi wa mabadiliko katika vijiji vyao.

Takwimu kutoka TANESCO zinaonesha kuwa nishati ya umeme ni nafuu zaidi kwenye matumizi ya upishi ikilinganishwa na mkaa au gesi, na pia ni salama kwa mazingira, hivyo kuchangia juhudi za kitaifa za kupunguza ukataji wa miti.

Kwa familia ya Samweta, jiko hilo limekuwa zaidi ya kifaa cha kupikia — limekuwa nyenzo ya amani, afya bora na mshikamano wa ndoa.

Share To:

Post A Comment: