NA DENIS MLOWE IRINGA 

TIMU za soka za Spana fc na BBC Fc zimekuwa timu za kwanza kufuzu hatua ya 8 bora katika mashindano ya kugombea kombe la Vunjabei baada ya michezo ya marudiano baina ya yao na timu za Migori Fc na Tanesco. 

Katika mchezo wa kwanza baina ya Spana fc na Migori timu ya Spana ilichezea kipigo cha goli 1 bila na mechi ya marudiano Spana fc waliondoka na ushindi wa goli 2 0 hivyo kufuzu moja kwa moja hatua ya nane bora. 

Wakati Spana wakifuzu timu ya BBC nayo imefanikiwa kufuzu hatua hiyo baada ya kutoka sare katika mchezo wa marudiano kwa matokeo ya 1 - 1 dhidi ya Tanesco wakati mchezo wa awali BBC walishinda goli 1.

Mashindano hayo yanaendelea leo ambapo zitapatikana timu mbili nyingine kufuzu hatua ya 8 bora kwenda kuwania kitita cha milioni 10 kinachotolewa na mdhamini wa mashindano hayo kampuji ya Vunja Bei chini ya Mkurugenzi wake Fred Ngajilo aka Fred Vunjabei .

Katika michezo ya leo Timu ya Isakalilo itakuwa mgeni katika uwanja wa shule ya Msingi Mlandege ambapo wenyeji wao watakuwa Viwengi ambapo katika mchezo wa kwanza timu ya Isakalilo ambayo hadi sasa haijawahi poteza mchezo itaingia na faida ya goli 5 ilizopata mechi ya kwanza.

Katika uwanja wa shule ya msingi Ipogoro kutakuwa ba mchezo mwingine katika ya Mti pesa dhidi ya Viwengi fc dhidi ya Kising’a fc ambapo timu mwenyeji anapewa nafasi kubwa kuingia hatua ya 8 bora baada ya ushindi katika mchezo wa kwanza.

Katika mashindano hayo mchezaji Barnaba Carlo amezidi kuwaacha mbali wapinzani wake katika kushindania mfungaji bora wa mashidano hayo baada ya kuwa na magoli 8 akifuatiwa na Osca Evaristo mwenye magoli matano.

Mashindano ya kombe la Vunjabei yamekuwa chachu ya mabadiliko ya soka mkoani Iringa na Nyanda za Juu Kusini kutokana na zawadi kubwa iliyowekwa kuliko mashindano yote kuanzishwa mkoani Iringa hivyo timu nyingi kuonyesha nia ya kuzinyaka fedha hizo.
Share To:

Post A Comment: