Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan leo Juni 16, 2025 akiwa ziarani Mkoani Simiyu amezindua shule ya Sekondari ya wasichana Simiyu, miongoni mwa shule 26 zilizojengwa kwenye Mikoa yote ya Tanzania bara ikiwa ni sehemu ya mpango wa Rais Samia wa kuboresha kiwango cha taaluma ya Sayansi kwa wasichana nchini.
Kulingana na Waziri wa nchi Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na serikali za Mitaa Mhe. Mohammed Mchengerwa, amebainisha kuwa katika kutekeleza dhamira ya Rais Samia, serikali ya awamu ya sita ilitoa takribani Bilioni 115.48 kwaajili ya ujenzi wa shule hizo 26, shule ambazo zimekamilika na zina wanafunzi takribani 9,810 kwasasa.
Kwa Mkoa wa Simiyu takribani Bilioni 4.45 zilitolewa na kutumika kwenye ujenzi wa shule hiyo ikihusisha Mabweni ya wanafunzi, viwanja vitatu vya michezo, nyumba tano za waalimu, Madarasa 22, maabara nne za Fizikia, Kemia, Baiolojia na Geografia, Jengo la utawala pamoja na Bwalo na Jiko lake lenye kutumia nishati safi ya kupikia.
Awali wakati akisoma taarifa hiyo kwaniaba ya Mkurugenzi Mtendajiwa Halmashauri ya Wilaya ya Bariadi,Mkuu wa Shule hiyo Mwalimu Huruma Mtindya amebainisha kuwa shule hiyo inatarajiwa kukamilika ujenzi wake mwishoni mwa mwezi huu, akieleza pia changamoto ya ukosefu wa samani kwenye bwalo la Chakula, Genereta na Gari ya shule, kama miongoni mwa changamoto zilizopo shuleni hapo.
Post A Comment: