Na  Issa Mwadangala

Wanafunzi wa Shule ya Sekondari Ivwanga iliyopo kata ya Mlowo Wilaya ya Mbozi Mkoani Songwe wameshauriwa kutumia vivuko vya watembea kwa miguu pindi wavukapo barabara au kuomba msaada kutoka kwa askari wa usalama barabarani ili kuepusha ajali zinazoweza kuepukika.

Rai hiyo imetolewa Mei 14, 2025 na Konstabo Maganga Kalulumya wa kikosi cha usalama barabarani Mkoani Songwe wakati alipokuwa akizungumza na wanafunzi wa shule hiyo na kuwaelimisha juu ya umuhimu na faidi ya kuvuka barabara katika vivuko vya watembea kwa miguu.

"Vivuko vya watemmbea kwa miguu ni sehemu salama zaidi kutokana na uwepo wa alama inayomtahadharisha dereva hivyo mnatakiwa kuacha tabia ya kuvuka maeneo yasiyo na vivuko kwani madereva hawachukui tahadhari juu ya watembea kwa miguu pasipo na kivuko" alisema Konstabo Maganga.

Pamoja na elimu hiyo Konstabo Maganga aliendelea kusisiza kuwa "ajali nyingi zinazotokea kwa watembea kwa miguu husababishwa na madereva wazembe ambapo hutokea maeneo ambayo hayana vivuko vya watembea kwa miguu hivyo amewataka kuchukua tahadhari pindi wavukapo barabara ili waendelee kuwa salama na kutimiza ndoto zao za baadae.

Naye kiongozi wa serikali ya wanafunzi wa shule hiyo Ester Said kwa niaba ya wanafunzi wenzake awali ya yote alilishukuru Jeshi la Polisi Mkoa wa Songwe kwa elimu waliyoipata na ameahidi kuzingatia ikiwa ni pamoja na kukumbushana pindi wamuonapo mwenzao ambaye afuati uvukaji salama pindi anapotaka kuvuka barabara ili waendele kuwa salama katika maisha yao ya kila siku.
Share To:

Post A Comment: