Wadau wa nishati safi kutoka nchi za Africa Mashariki na mataifa jirani wamekutana mkoani Arusha katika kongamano la nishati safi ya kupikia,likihusisha kubadilishana uzoefu katika matumizi ya majiko ya kisasa ya kupikia ili kuiwezesha jamii kuondokana na matumizi ya nishati zisizo salama ikiwemo matumizi ya kuni.

Akizungumza kwa niaba ya Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa nishati katika ufunguzi wa kongamano hilo Kamishna wa umeme na nishati Jadidifu Mhandisi Innocent Luoga amebanisha azma ya serikali ni kushirikiana na wadau na wabunifu kutoka Taasisi binafsi zenye kubuni matumizi ya nishati mbadala ambazo ni safi za kupikia.

"Tumeendelea kugawa mitungi lakini kama tunavyofahamu nishati ya kupikia sio mitungi pekee,na sasa hivi tunaendelea kutoa elimu kwa wananchi kutumia nishati ya umeme kwa sababu umeme ni nishati safi na ni rahisi kutumia,na hii ni kwa sababu tuna teknolojia. Kwa hiyo tumekutana haoa ili kubadilishana uzoefu" Alifafanua Kamishna wa umeme na nishati Jadidifu kutoka Wizara ya nishati Eng. Innocent Luoga.

Shirika la viwango Tanzania TBS ni moja ya mashirika na wadau wa nishati safi waliojitokeza katika kongamano hilo,wakiwa na jukumu la kudhibiti viwango sahihi kwenye Teknolojia mbalimbali za majiko ya kisasa ya kupikia ili kuhakikisha usalama kwa watumiaji. 

"Inatakiwa kuwepo viwango katika kuendana na nishati safi ya kupikia ili kuhakikisha hiyo asilimia 80% inafikiwa kwa maana ya kwamba mtumiaji abaki akiwa salama na mazingira yakiwa salama pia,Tumeona Teknolojia mbalimbali  za majiko ya kupikia kuonyesha ufanisi wa majiko haya mzalishaji anatakiwa kuonyesha ni kwa namna gani haya majiko yanafanya kazi,na anaweza akasema ufanisi wa majiko haya ni kwa asilimia 90%  sasa kama TBS hajasimama na kueleza majiko haya ufanisi wake ni kwa asilimia 80% basi Mwananchi ataibiwa"  Alifafanua Mhandisi Adson Kagaba muhandisi wa umeme kutoka Shirika la viwango TBS.

Kongamano hilo litakalo fanyika kwa muda wa siku tatu mkoani Arusha litakutanisha wataalamu na wabunifu wa Teknolojia mbalimbali za majiko na kujadili ni kwa namna gani Mwananchi anaondokana na matumizi ya nishati zisio salama.








Share To:

Post A Comment: