CHAMA cha Wafanyakazi wa Vyombo vya Habari Tanzania (JOWUTA), leo kimetangazwa rasmi kuwa mwanachama wa Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi nchini (TUCTA).

Aidha, Rais Samia Suluhu Hassan ametangaza neema kwa wafanyakazi wa serikali kwamba kuanzia Julai 2025 mshahara utaongezeka kwa asilimia 35.1 na kuwezesha wafanyakazi wa kima cha chini kulipwa shilingi 500,000 kutoka 370,000 ya sasa.

Taarifa hiyo ya kufurahisha kwa JOWUTA imetolewa na Katibu Mkuu wa TUCTA, Henry Nkunda, wakati wa akisoma risala ya wafanyakazi mbele ya Rais Samia, kwenye maadhimisho ya sherehe za Mei mosi Kitaifa zilizofanyika kwenye Viwanja vya Bombadia mjini Singida leo.

Nkunda alisema pamoja na JOWUTA vyama vingine ambavyo nimepokelewa kama wanachama wapya ni Chama cha Wafanyakazi wa Kampuni Binafsi za Ulinzi nchini (TUPSE) na Chama cha Wafanyakazi za Huduma za Viwandani Tanzania (TASIWU).

Baada ya vyama hivyo vitatu kuwa mwanachama rasmi wa TUCTA sasa itakuwa na jumla ya vyama vya wafanyakazi  wanachama 16.

"Mheshimiwa Rais TUCTA ilipokea maombi ya vyama tisa vya wafanyakazi ambapo baada ya Bazara Kuu kukutana na kujadili vyama vitatu vya JOWUTA, TUPSE na TASIWU vimefanikiwa kukidhi vigezo na kujiunga na shirikisho hili, bado tunaendelea na mchakato wa kuunga vyama vingine , lengo letu ni kuwa wamoja," alisema.

Akizungumza mjini hapa na viongozi wa JOWUTA ,Rais wa TUCTA Tumaini Nyamuhokya alipongeza JOWUTA vyama vingine kudumisha ushirikiano na kufanya kazi na shirikisho kwa maslahi ya wanachama.

"Mimi muda mrefu nilikuwa napenda JOWUTA mkamilishe taratibu na kuwa wanachama wa TUCTA ili tusaidiane kusaidia tasnia yenu"alisema

Mwenyekiti wa Taifa wa JOWUTA, Mussa Juma alimweleza Rais huyo wa TUCTA kuwa JOWUTA imepokea kwa furaha kubwa tangazo la kukubaliwa kuwa mwanachama wa shirikisho.

Alisema JOWUTA itajitahidi kufuata taratibu na Kanuni za TUCTA, ili kuwa mwanachama hai na hivyo kushirikiana kutatua changamoto katika tasnia ya habari nchini.

"Tunashuru sana kukubaliwa maombi yetu ya muda mrefu kuwa mwanachama wa TUCTA na sasa tunaimani kwa kutumia uzoefu wa TUCTA katika kushughulika na masuala ya kazi, ili wafanyakazi wa vyombo vya habari wanufaike"alisema

Naye Katibu wa JOWUTA Selemani Msuya alisema chama hicho kukubaliwa kujiunga  TUCTA ni ushahidi tosha kwamba linapambania maslahi ya wanachama wake na kuwataka wanachama wake walipe ada kwa wakati ili kujenga ushirikiano huo.

"Hii ni habari njema kwetu sisi JOWUTA, napenda kutumia nafasi hii kuwaomba wanachama walipe ada kwa wakati na waandishi wengine wajiunge ili kuwa na nguvu pamoja katika kupigania maslahi yetu," alisema.

Akizungumzia vyama vya wafanyakazi Rais Samia alivitaka viwe chachu ya maendeleo na kuzingatia sheria za kazi ambao wanaosimamia.

Katika madhimisho ya Mei Mosi mwaka huu, Rais Samia ametangaza nyongeza ya mishahara ya kima cha chini kwa asilimia 35.1 wafanyakazi wa serikali ambapo watakuwa wanalipwa mishahara wa shilingi 500,000 kutoka shilingi 370 ,000 kuanzia Julai mosi 2025.

Alisema kwa sekta binafsi mchakato wa nyongeza unaendelea kupitia bodi ya mishahara ya sekta binafsi.

Rais Samia amesema.serikali imefikia uamuzi huo.baada ya uchumi kuanza kuimarika kutokana na kuongezeka uzalishaji nchini.

Alisema uchumi kwa sasa umefikia asilimia 5.5 kutoka 4.6 mwaka 2024, hivyo anaona ni wakati muafaka wa kuongeza mshahara.

Tangazo hilo la Rais lilipokewa kwa shangwe na nderemo na maelfu ya wafanyanyakazi waliokuwa wamejitokeza anbao swali walionekana kupoa kiwanjani hapo.

Waziri wa Ajira, Kazi na Watu wenye Ulemavu, Ridhiwani Kikwete alisema atahakikisha utatu unasimamiwa katika wizara yake ili kila upande uweze kunufaika.






Share To:

Post A Comment: