Serikali ya Awamu ya sita kupitia kwa Wizara ya Ujenzi imeliambia Bunge la Tanzania leo Mei 06, 2025 kuwa kwasasa unafanyika usanifu wa kina kwenye Barabara ya Chalinze- Segera Mkoani Tanga ili kuanza upanuzi wa barabara hiyo muhimu kwa uchumi wa Tanga na mikoa ya Kaskazini mwa nchi.
Waziri Abdallah Ulega anayesimamia Wizara ya Ujenzi amebainisha hayo muda mfupi uliopita wakati akihitimisha Mjadala wa Hotuba ya Bajeti ya wizara yake kwa Mwaka wa fedha 2025/26, akieleza kuwa serikali inatambua kuwa barabara hiyo imekuwa finyu kwasasa kutokana na wingi wa matumizi yake kwasasa kutokana na kujengwa miaka mingi iliyopita, hivyo kushindwa kukidhi haja na matarajio ya sasa.
Waziri Ulega ameeleza hayo kufuatia hoja na ushauri kadhaa uliotolewa na Wabunge Akiwemo Mhe. Ummy Mwalimu na Mhe. Rashid Abdallah Shangazi walioomba barabara hiyo kutazamwa kwa kina na Wizara ambapo Mhe. Ulega ameahidi kuwa mara baada ya usanifu, mchakato utakaofuata ni kutafuta fedha kwaajili ya Ujenzi wa barabara hiyo.
Post A Comment: