Waziri wa Ujenzi nchini Tanzania Mhe. Abdallah Ulega akihitimisha mjadala wa Bajeti ya Wizara yake kwa mwaka wa fedha 2025/26 amewaelekeza wataalamu wa Wizara hiyo kufanya tathmini ya barabara zilizoombwa na wabunge kuweza kupandishwa hadhi.

Mhe. Ulega katika maelezo yame amesisitiza kuwa atahakikisha Majibu yanapatikana kabla ya Bunge kuisha muda wake mwezi Julai mwaka huu.

"Zipo taratibu za upandishaji hadhi barabara hizi ukijumuisha kufanya tathmini na ipo kamati ya kiserikali ambayo yenyewe hushughulika na kuangalia vile vigezo kwahiyo nawaagiza wataalamu wangu hapa wachukue hizi barabara zilizosemwa hapa na waheshimiwa Wabunge, ninataka niwahakikishie tunakwenda kulifanyia kazi jambo hili na tutayapata majibu kabla bunge hili halijafika mwisho wake"

Katika hatua nyingine Waziri Ulega amezungumzia hoja ya Baadhi ya Wabunge kueleza kuwa baadhi ya Wakandarasi wamekuwa hawalipwi stahiki zao kwaajili ya ujenzi wa miradi mbalimbali nchini, ambapo ameliambia Bunge kuwa Wizara yake kwa kushirikiana na Wizara ya fedha watahakikisha mkandarasi anayetekeleza ujenzi wa barabara ya Ifakara-Chita na barabara ya Bigwa-Kisaki anapewa kipaumbele katika fedha ambazo zitapatikana hivi karibuni ili kuwezesha utekelezaji wa miradi kuweza kuendelea.

Share To:
Next
This is the most recent post.
Previous
Older Post

Post A Comment: