Waziri wa Ujenzi, Abdallah Ulega amewasisitiza watumishi wa Wizara ya Ujenzi na taasisi zake kufanya kazi usiku na mchana na kwa moyo dhati ili kuleta maendeleo nchini kupitia Sekta ya Ujenzi.
Ameyasema hayo leo Mei 07, 2025 jijini Dodoma katika kikao cha majumuisho kufuatia kupitishwa Bungeni kwa bajeti ya Wizara hiyo kwa mwaka wa fedha 2025/2026.
“Ni wakati wa kuchapa kazi, kuendelea kutekeleza miradi na kupeleka huduma kwa watu kupitia barabara, madaraja, vivuko na nyumba, na hii ndio maana halisi ya ‘kazi na utu’, amesema Ulega.
Aidha, Ulega, ametoa rai kwa watumishi hao kufanya kazi kwa kuzingatia weledi, uadilifu na ushirikiano ili kupata mustakabali mzuri wa utendaji kazi wa Wizara na Taasisi zake kwa ujumla.
Kikao hicho kimeshirikisha Vingozi wakuu wa Wizara, Menejimenti ya Wizara, Wakuu wa Taasisi zilizo chini ya Wizara na watumishi mbalimbali kutoka wizara hiyo na Taasisi zilizo chini ya Wizara.
Post A Comment: