Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan leo Jumapili Machi 09, 2025 anatarajiwa kuwa Mkoani Kilimanjaro ambapo pamoja na mengine, anatarajiwa kuwa Nyumba ya Mungu, Wilayani Same kuzindua mradi wa maji Same-Mwanga-Korogwe.

Mradi wa maji Same-Mwanga-Korogwe ulisanifiwa mwaka 2008 ambapo serikali kwa kushirikiana na wadau mbalimbali wakiwemo Arab Bank for Economic Development in Afrika na wadau wengineo walilenga kujenga mradi mkubwa wa maji kwaajili ya kuhudumia wakazi wa Miji ya Same na Mwanga na Vijiji 38 vya Wilaya ya Korogwe ili kuondokana na changamoto iliyokuwepo awali.

Mradi hyo umetumia takribani Bilioni 300 kwa awamu ya kwanza na kwasasa kazi zinazoendelea ni pamoja na kuendeleza mtandao wa mabomba na kufanya maunganisho ya maji kwa wananchi, kukarabati na kuboresha miundombinu ya maji chakavu ikiwa ni pamoja na kubadilisha mabomva makubwa kulinganisha na mahitaji, kazi ambazo kufikia April 2025 huduma ya maji inatarajiwa kuwa imewafikia wananchi walengwa kwa asilimia 95.

Kukamilika kwa mradi huo wa Maji Same-Mwanga-Korogwe kunatajwa na serikali kuwa kutapelekea uwepo wa maji ya kutosha Mjini Same na Mwanga hivyo kutoa fursa kwa wawekezaji kuchangia kukuza uchumi wa maeneo hayo na Kilimanjaro kaa ujumla kwani upatikanaji wa maji utakuwa ni wa uhakika kwa saa 24 kutoka saa sita kwa siku zilizokuwepo awali.











Share To:

Post A Comment: