Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Mhe. Omary Juma Kipanga amesisitiza Taasisi kutoa kipaumbele kwenye afya na ustawi wa akili kwa kuweka mazingira mazuri na kuhamasisha mbinu bora za kukabiliana na msongo wa mawazo ili kutokuathiri kazi, maamuzi na malengo ya muda mrefu ya Taasisi.


Mhe. Kipanga ameyasema hayo wakati akifungua mafunzo ya siku mbili ya Menejimenti ya Taasisi ya Afrika ya Sayansi na Teknolojia ya Nelson Mandela yaliyoandaliwa kwa uratibu wa na Mradi wa Elimu ya Juu kwa Mageuzi ya Kiuchumi (HEET).

“Naishukuru sana Wizara kupitia mradi wa HEET na uongozi wa taasisi kwa kuona umuhimu wa mafunzo haya kwa wajumbe wa Menejimenti na kuyatoa kwa wakati” amesema Mhe. Kipanga

Kwa Upande wake Makamu Mkuu wa Taasisi ya Afrika ya Sayansi na Teknolojia ya Nelson Mandela Prof. Maulilio Kipanyula ameeleza kuwa, mafunzo hayo ni utekelezaji wa matakwa ya mradi wa HEET ya kuwafundisha washiriki kutambua na kuwasaidia watu wenye mahitaji maaluum, afya ya akili, jinsia, ukatili na unyanyasaji wa kijinsia ili kutoa huduma bora kwa wadau.

Mradi wa HEET umejikita katika kutoa mafunzo Madhubuti kwenye masuala ya Kijinsia kwa kutengeneza Sera ya Jinsia (Gender Policy), kuunda Dawati la Jinsia (Gender Desk) pamoja na kutumia mfumo wa Serikali wa e-Mrejesho kupokea na kutuma malalamiko, pongezi pamoja na maoni.
Share To:

Post A Comment: