Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Malinyi Bi. Rose Robert Manumba ameongoza timu ya Wataalam kutoka Halmashauri kusikiliza na kujibu Kero za Wananchi katika mkutano wa hadhara uliofanyika Kata ya Njiwa.

Kero mbalimbali zilizoibuliwa na Wakazi wa njiwa ni pamoja na  kutaka ufafanuzi wa huduma za afya,

Migogoro mbalimbali ya ardhi kati ya vijiji, taasisi na mtu mmoja mmoja,Stakabadhi ghalani, hatma ya vitongoji halali vilivyopo maeneo ya hifadhi,Migogoro ya wakulima na wafugaji.

Baadhi ya kero hizo zilipatiwa majibu ya hapo kwa hapo na Mkurugenzi pamoja na Wataalam kutoka Halmashauri na nyingine Mkurugenzi Aliahidi kuwasilana na Tasisi husika na atawarejea Wananchi kwa majibu ndani ya muda mfupi.

"Niwahakikishie Wananchi wa Njiwa yale yote niliyoyachukua kwaajili ya utekelezaji nitaenda kuyasimamia ipasavyo,kuna yale ambayo nimeyatolea muda kwaajili ya  utekelezaji  nitatimiza ahadi yangu, na hata yale ambayo sikuyatolea muda niwahakikishie kwamba naenda kufanya ufuatiliaji wa kina kuhakikisha kwamba yanatekelezwa ili kuondoa kero na changamoto zote zinazowakabili na kuhakikisha ufumbuzi unapatikana" amesema Mkurugenzi Manumba

Aidha Mkurugenzi amewataka Watumishi katika Kata ya Njiwa kutekeleze majukumu yao  kwa uaminifu na uadilifu, kuzingatia kanuni na miongozo yote inayowataka kutekeleze majukumu yao  kikamilifu kama Watumishi.

Hata hivyo, Mkurugenzi Manumba amewashukuru Wananchi wa Kata ya Njiwa kwa kushiriki  kwa wingi katika mkutano huo  na kuainisha changamoto  mbalimbali zinazo wakabili na amewaomba Wananchi hao kuendelea  kushirikiana  na kutoa taarifa mbalimbali  katika Ofisi ya Mkurugenzi.

Share To:

Post A Comment: