Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Malinyi Bi. Rose Robert Manumba amewataka Watumishi katika Kata ya Njiwa kutekeleze majukumu yao kwa uaminifu na uadilifu na kuzingatia matumizi Bora ya fedha za Serikali Aidha Mkurugenzi amewashukuru Wananchi wa Kata ya Njiwa kwa kushiriki kwa wingi katika mikutano na kuainisha changamoto mbalimbali zinazo wakabili na amewaomba Wananchi hao kuendelea kushirikiana na kutoa taarifa mbalimbali katika Ofisi ya Mkurugenzi

"Niwahakikishie Wananchi wa Njiwa yale yote niliyoyachukua kwaajili ya utekelezaji nitaenda kuyasimamia ipasavyo,kuna yale ambayo nimeyatolea muda kwaajili ya utekelezaji nitatimiza ahadi yangu, na hata yale ambayo sikuyatolea muda niwahakikishie kwamba naenda kufanya ufuatiliaji wa kina kuhakikisha kwamba yanatekelezwa ili kuondoa kero na changamoto zote zinazowakabili na kuhakikisha ufumbuzi unapatikana" amesema Mkurugenzi

Share To:

Post A Comment: