Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Balozi Dkt Emmanuel John Nchimbi akizindua Shina la Wakereketwa Wajasiriamali wa Tarime Group, lenye wanachama 200, eneo la Makuyuni, Wilaya ya Monduli, mkoani Arusha.


Balozi Nchimbi amewasili na kupokelewa Arusha leo Jumapili, Juni 2, 2024, tayari kuanza ziara ya siku tatu mkoani humo, ikiwa ni mwendelezo wa ziara yake kwenye mikoa mitano, ya Singida, Manyara, Arusha, Kilimanjaro na Tanga, akiwa amembatana na Katibu wa NEC, Itikadi, Uenezi na Mafunzo CPA. Amos Makalla pamoja na Katibu wa NEC, Siasa na Uhusiano wa Kimataifa (SUKI), Ndugu Rabia Hamid Abdallah.Share To:

Post A Comment: