Na Dickson Mnzava,Same.

Chama cha Mapinduzi CCM Wilayani Same Mkoani Kilimanjaro kimetoa semina na mafunzo ya ungozi kwa mabalozi na viongozi wa mashina 1015 katika tarafa za Ndungu, Mamba Vunta na tarafa ya Gonja lengo likiwa ni kuwajengea uwezo zaidi wa uelewa wa majukumu yao hususani kipindi hiki cha kuelekea kwenye uboreshaji daftari la wapiga kura sambamba na uchaguzi wa serikali za mitaa.


Akizungumza kwenye semia hiyo katika tarafa ya Gonja mwenyekiti wa CCM Wilayani Same Mkoani Kilimanjaro Abdullah Suleiman Mnyambo amesema wameamua kutoa semina kwa viongozi hao ili waweza kuwa chachu ya kuwaelezea wananchi umuhimu wa kujiandikisha na umuhimu wa kushiriki kwenye chaguzi mbalimbali za serikali za mitaa.


Mnyambo amesema mafunzo kwa Viongozi hao yanaenda pia kuelezea mafanikio ya serikali ya Chama Cha mapinduzi chini ya Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan namna ambavyo ameweza kutoa fedha nyingi za miradi mbalimbali ya maendeleo kwa wananchi wa Jimbo la Same mashariki.

"Kiukweli tumefanikiwa kwakiasi kikubwa watu 1015 si haba ukizingatia kila balozi ana watu zaidi ya 30 hivyo mabalozi hawa kwa idadi yao kila mmoja akishuka kutoa elimu kwa watu wake 30 tutakuwa tumefanikiwa kwa kiasi kikubwa sana na wananchi wetu wataweza kusikia na kuona mafanikio ya serikali kwao lakini pia waweza kujitoa kugombea nafasi mbalimbali za uongozi kwenye chaguzi za serikali za mitaa"

"Alisema mwenyekiti CCM Same Mnyambo". 


Akisoma utekelezaji wa ilani ya Chama Cha Mapinduzi kwa viongozi wa Chama hicho Mbunge wa jimbo la Same mashariki Anne Kilango amesema wamefanikiwa kutekeleza ilani kwa zaidi ya asilimia 85 hadi kufikia sasa huku akisema bado ipo miradi mingine ambayo inaendelea kutekelezwa kwenye jimbo hilo hivyo watafikia zaidi ya asilimia 100.


Amesema serikali ya awamu ya sita imeweza kuboresha miundombinu ya barabara ya Same,Mwembe,Mhezi,Mbaga,Bombo hadi Miamba ambapo jumla ya madaraja 8 yamejengwa kwa kipindi hiki na kurahisisha huduma ya mawasiliano kwa wananchi wa Tarafa ya Gonja.

Kilango amesema kukutana na viongozi hao kwaajili ya mafunzo sambamba na kusoma ilani ya Chama Cha Mapinduzi ni kutaka kuwapatia wananchi taarifa ya utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo ambayo imekuwa ikitengewa fedha Kutoka serikali kuu chini ya Rais Samia.


Amesema miongoni mwa changamoto kubwa ambazo zilikiwa kikwazo kwa wananchi wa kanda za milimani kwenye Jimbo lake ni huduma za Afya na ubovu wa miundombinu ya barabara kitu ambacho sasa kimepatiwa muarobaini na serikali kwani Vituo 3 vya afya vimejengwa katika tarafa za Mamba Vunta na tarafa ya Gonja ukanda huo wa milimani.


 

Share To:

ASHRACK

Post A Comment: