WATUMISHI RORYA WALIPWA MISHAHARA YAO.
WATUMISHI ZINGATIENI MIFUMO YA KIUTENDAJI.
Serikali imeshawalipa watumishi zaidi ya 700 wa Wilaya ya Rorya mkoani Mara ambao walishindwa kuingia kwenye mfumo wa usimamizi wa utendaji kazi katika utumishi wa umma PEPMIS baada ya kutokea kwa changamoto mbalimbali ambazo zingine zimesababishwa na watumishi wenyewe kutojisajili kwenye mfumo huo.
Leo tarehe 16.05.2024 kwa njia ya simu Mbunge wa Rorya Mhe.Chege amemueleza Naibu Waziri Utumishi Mhe.Kikwete kuwa watendaji wameshaanza kuona na kupokea miamala ya mishahara yao na tatizo limeshatatuliwa hivyo hakuna malalamiko mengine waliyoyapokea kutoka kwa watumishi Wilayani humo ya kukosa stahiki zao za mishahara.
Mapema jana Bungeni Jijini Dodoma Naibu Waziri Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe.Ridhiwani Kikwete akijibu swali la Mbunge wa Rorya Jafari Chege ,aliliambia Bunge kuwa changamoto iliyotokea Wilaya ya Rorya kwa baadhi ya watumishi kukosa mshahara wa mwezi wa tatu , ilisababishwa na watumishi hao kutojiorodhesha wenyewe kwenye jedwari la kiutendaji kama ambavyo imeelekezwa na serikali.
Mhe. Kikwete alisema “muongozo wa serikali ulishaelekeza watumishi wote ambao hawakujiorodhesha kwenye jedwari la kiutendaji wanatakiwa wafungiwemishahara yao na taratibu zilifanyika lakini baada ya maeneo yalionekana kuna changamoto mbalimbali zikiwemo taarifa ambzao zimeletwa” alijibu Mhe.Kikwete.
“Mhe. Mwenyekiti Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi na Utawala Bora nakulifanyia kazi jambo hilo na tayari imepekea ombi jipya kwaajili ya utatuzi wa hiyo kero nyingine ya mishahara ambayo kupitia wizara ya fedha wanategemea kupata fedha hizo na hilo jambo linategemewa kuisha wiki hii na nina muhakikishia Mhe.Mbunge kwamba asiwe na wasiwasi watumishi wake watarudishiwa malipo ya mishahara yao na mambo yataenda vizuri” alisisitiza Mhe. Kikwete
Katika hatua nyingine Mhe.Kikwete ametoa angalizo kwa watumishi wa halmashauri zote, watumishi wote chini ya serikali kuu na serikali ya mitaa wajiorodheshe na wajiunge na mfumo huo ili serikali iendelee kupima utendaji wao wa majukumu yao kama serikali inayoongozwa na Mhe. Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan inavyoelekeza.
Post A Comment: