Mkuu wa Mkoa wa Njombe Mheshimiwa Anthony Mtaka amekemea vikali kufanyika kwa shughuli za kibinadamu ikiwemo kulisha mifugo pamoja na kufanya kilimo kwenye vyanzo maji.

Hayo yamejiri kwenye ziara aliyoifanya Wilaya ya Ludewa kata ya mavanga, kijiji cha mavanga ambapo wananchi wililamikia uchafu wa maji kwenye mradi unatekelezwa kijijini hapo wenye thamani ya zaidi ya bilioni 1.3 utakaohudumia wakazi wapatao 5,000

“Ni kweli dinga zipo,lakini maji yanachafuliwa na shughuli za kibinadamu ,mtashikana uchawi bure lakini wachawi ni sisi wenyewe ,Mhe. Rais ameshatimiza wajibu wake fedha zimefika,wekundu wa maji unasababishwa na ngo’mbe” Alisema Mhe. Mtaka.

Awali mmoja wa wananchi wa kijiji hicho m Musa mwabena aliishukuru Serikali kwa mradi huo lakini alilalamikia changamoto ya maji mradi huo kutoka yakiwa machafu hali ambayo inahatarisha afya zao. 

Mhe. Mtaka ametoa wito kwa Viongozi wa kijiji na kata kushirikiana  katika kujiwekea sheria ndogondogo kwa ajili ya kulinda vyanzo vya maji kwa faida ya kijiji na taifa kwa ujumla.

“Kwenye WADC wekeni sheria ,mkitaka mtusaidie watu wenye ngo’mbe kwenye eneo la chanzo watoe ngo’mbe ,watu wanaolima kule karibu na chanzo watoke,kwa sababu kuna siku mradi utakamilika maji yatakuwa hayatoki chanzo kitakuwa kimekauka.”Alisisitiza

Aidha amempongeza  mkandarasi mzawa anaetekeleza mradi huo Emirate Builders Co. Ltd kwa kuonesha uzalendo.

“Tunahitaji wakandarasi  kama Emirate ametekeleza  mradi mpaka hatua hii kwa malipo ya asilimia 15,tungekuja hapa tukute mawe mashimo na picha nzuri ya tenki la maji lakini ametumia fedha ya mtaji wake ,lakini pia amekubali  maboresho ya nyongeza,mnapopata miradi mingine watu wa hivi wapeni .”

Kwa upande wake kaimu Meneja wa Wakala wa Maji na Usafi wa Mazingira Vijijini Wilaya ya Ludewa, Mwita Isaya  alisema utekelezaji wa mradi huo wa kijiji cha Mavanga unalenga kuimarisha miundombinu ya mradi wa awali kwa kujenga miundombinu mipya, kupanua mtandao wa maji na kuongeza huduma ya maji kutoka kwenye chanzo kipya cha mto Msolwa







.

Share To:

Post A Comment: