Wizara ya Afya imepanga kutekeleza vipaumbele 10 kwa kutumia afua 86 zinazokadiriwa kutumia kiasi cha shilingi 1,311,837,466,000 kwa mwaka ujao wa fedha 2024/25 itakayohusisha mapato, matumizi ya kawaida na miradi mbalimbali ya maendeleo kwa mwaka huo Hayo yamebainishwa leo, Jumatatu Mei 13.2024 na Waziri wa Afya Mhe. Ummy Mwalimu wakati akiwasilisha Hotuba ya makadirio ya mapato na matumizi ya Wizara hiyo kwa mwaka wa fedha 2024/25 Bungeni jijini Dodoma kupitia Bunge la 12, Mkutano wa 15, Kikao cha 24 ambapo ametaja vipaumbele hivyo kuwa ni pamoja na kuimarisha huduma za kinga dhidi ya magonjwa ambapo katika eneo hilo kiasi cha shilingi 117, 611,588,304 kimetengwa Vipaumbele vingine ni pamoja na kuimarisha upatikanaji wa ubora wa huduma za afya zinazotolewa na vituo vya kutolea huduma za afya katika ngazi zote ambapo jumla ya shilingi 219,010,767,716 zimetengwa ili kutekeleza eneo hilo, sambamba na hilo liko suala la kuimarisha huduma za afya za uzazi, mama na mtoto ambapo kwenye eneo hilo kiasi kilichotengwa ni shilingi 17,189,250,000 Waziri Ummy ametaja vipaumbele vingine kuwa ni pamoja na kuimarisha upatikanaji wa wataalam katika sekta ya afya katika fani za kati, ubingwa na ubingwa bobezi ambapo kwenye eneo hilo kiasi kilichotengwa ni shilingi 74,000,000,000, hiyo ikienda sambamba na kuimarisha huduma za matibabu ya ubingwa na ubingwa bobezi nchini ambapo kiasi kilichotengwa kwenye eneo hilo ni shilingi 89,858,609,000 Aidha, katika vipaumbele hivyo lipo suala la kuendeleza na kusimamia afua za Tiba Asili na Tiba Mbadala ambapo kiasi cha shilingi 1,500,000,000 kimetengwa, kuimarisha udhibiti wa magonjwa ya kuambukiza, magonjwa yasiyoambukiza, magonjwa ya mlipuko na huduma za afya za dharura ambapo kwenye eneo hilo Wizara imetenga kiasi cha shilingi 84,864,241,569, na kuimarisha huduma za afya ya akili ambapo kiasi kilichotengwa kwenye eneo hilo ni shilingi 5,618,528,988 Pia, Wizara ya Afya imegusia suala la kuimarisha huduma za utengamao na tiba shufaa hususani kwa watoto, wazee na wenye ulemavu ambapo kiasi kiasi cha shilingi 3,700,000,000 kimetengwa kwenye eneo hilo Vipaumbele vingine vilivyowekwa na Wizara ya Afya kwa mwaka ujao wa fedha ni pamoja na kusimamia tafsiri na matumizi ya matokeo ya tafiti mbalimbali za afya ambapo kiasi kilichotengwa ni shilingi 3,508,968,000, pamoja na kuimarisha mifumo ya ugharamiaji wa huduma za afya nchini ambapo kiasi kilichotengwa kwenye eneo hilo ni shilingi 6,000,000,000
Share To:

Post A Comment: