Meneja wa RUNALI Jahida Hassan akiongea na wadau mbalimbali pamoja na viongozi wa AMCOS kutoka wilaya ya Nachingwea, Ruangwa na Liwale wakati wa mafunzo kwa viongozi hao
Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya Nachingwea Adinan Mpyagila akiongoza zoezi la ugawaji wa vifungashio vya mazaoBaadhi ya washiriki wa mafunzo yanayotolewa na RUNALI 


CHAMA kikuu cha ushirika (RUNALI) kimegawa jumla ya viroba laki 800,000, vitabu pamoja na kamba kwa wakulima wa wilaya ya Nachingwea, Ruangwa na Liwale kuelekea msimu wa mauzo ya mazao ya ufuta,Mbazi na Korosho.

Akizungumza wakati wa uzinduzi wa ugawaji wa vifungashio hivyo, meneja wa RUNALI Jahida Hassan alisema kuwa wamegawa vifungashio hivyo kwa lengo la kuwawezesha wakulima kuhifadhi mazao kwenye ubora unaotakiwa sokoni.

Hassan alisema kuwa RUNALI wamekuwa wanatoa elimu mara kwa mara kwa wakulima ili waweze kulima kilimo kilicho bora na kufanikiwa kupeleka mazao yaliyo bora sokoni.

Alisema wapo tayari kwa kuanza msimu mpya wa Mbaazi na ufuta na lengo la mafunzo haya ni kuwajengea utayari wa kwenda kwenye msimu mpya pia wametoka kifahamishana umuhimu wa kufanya ukaguzi.

Licha ya kutoa vifungashio hivyo lakini RUNALI walitoa mafunzo kwa wenyeviti na makatibu 212 ambapo mgeni rasmi alikuwa mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Nachingwea Adinan Mpyagila kuwataka viongozi waliopata mafunzo kwenda kutoa elimu kwa wajumbe wa bodi na makalani katika vyama vyao.

Mpyagila amewasihi wakulima kutouza mazao kiholela na kuweka vituo kwenye mipaka ya wilaya ili mazao yasiuzwe nje ya wilaya kwa kuwa itapelekea kupoteza mapato ya Halmashauri kwenye mazao ya mbaazi na ufuta.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa chama cha ushirika (RUNALI) Odas Mpunga amewapongeza vyama vya Ushirika kwa kazi kubwa waliyofanya na kuingiza mapato makubwa. Pia, amewataka kuyatumia vema mafunzo haya kwa vitendo ili kuleta Matokeo chaya.



Share To:

mwangaza wa hbari

Post A Comment: