Na Ashrack Miraji Same Kilimanjaro 

mbunge wa Jimbo la Same magharibi Mhe David Mathayo ameuliza swali la nyongeza Kwa Mhe Waziri wa Aridhi Jerry Slaa kumtaka ni lini atakwenda kutatua Kero na migogoro ya Aridhi Inayoendelea katika Kijiji Cha Bangalala tarafa ya mwembe- Mbango kata ya Makanya na Ruvu katika wilaya ya Same ambayo inapelekea kukwamisha Maendeleo ya Wananchi hasa katika kipindi hichi Cha kilimo na ufugaji.


"Nikuombe Mhe Waziri naomba tuongozane pamoja baada ya vikao vya bunge kumalizika kwenda Kutatua Migogoro hiyo ambayo imedumu Zaidi ya miaka 19 bila ya ufumbuzi wowote na Kupelekea Wananchi kutoelewana na kusimamisha shughuli za Maendeleo katika maeneo hayo lengo Wananchi Hawo waweze kuishi Kwa amani na upendo kuendelea kufanya shughuli zao za kiuchumi"

" Amesema Mathayo" 


Waziri Mwenye dhamana ya Aridhi Mhe Jerry Slaa amekiri kuambatana na Mhe Mbuge wa jimbo la Same Magharib David Mathayo mara baada ya kumaliza kuwasilisha bajeti yake ya wizara ya Aridhi ifikapo Mwezi June Mwaka huu kwenda Kutatua Migogoro hiyo ambayo inaendelea katika kipindi hiki 


"Mhe Mwenyekiti niiombe radhi Kwa Wananchi wa Same hasa Wa jimbo la Same Magharibi ambao nilifanya ziara January 26 na kutembelea sehemu ya migogoro hiyo Kata ya Bangalala Makanya na Ruvu na pia nikatuma watahalam kuja kupima maeneo na mipaka nimeshawasilishiwa ofisini hivyo Baada ya kumalizika Kwa vikao vya bunge ntaongozana na Mhe Mbuge David Mathayo kwenda Kutatua Migogoro hiyo"

" amesema Mhe Jerry Slaa".


Mwisho.

Share To:

ASHRACK

Post A Comment: